Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kimeandaa kongamano la tatu la mwaka la kimataifa, litakalozungumzia dhana nzima ya uchumi wa buluu.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa chuo hicho Dkt Tumaini shaabani Gulumo amesema kongamano hilo,litafanyika kuanzia Julai 4 hadi 5, 2024, jijini, Dar es Salaam, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Gulumo amesema chuo chao kikishirikiana na kile Cha Reginal Maritane University Cha nchini Ghana kimeandaa mkutano huo wenye lengo la kutafsiri dhana nzima ya uchumi wa buluu ambapo Tanzania imepewa heshima kubwa ya kuandaa kongamano hilo.
Aidha Dkt, Gulumo ametoa ufafanuzi juu ya dhana nzima ya uchumi wa buluu ikiwemo shughuli nyingi zinazofanyika baharini, ikiwemo sekta ya uchukuzi, uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi, utalii na kilimo Cha mwani na nyinginezo.
Katika hatua nyingine Gulumo amesema mbali na mambo mengine yatakayojadiliwa kwenye kongamano hilo ni pamoja na usalama wa bahari ikiwemo uharamia, matumizi mabaya ya baharini ikiwemo uharibifu wa mazingira.
Dkt, Gulumo ameendelea kusema kuwa Chuo Cha Bahari kikiwa chuo pekee hapa nchini kilichopewa mamlaka kumsimamia mambo yote yanayohusu uchumi wa buluu bila kuangalia vyanzo vingine vya maji vilivyopo nchini.
Amesema kwa sasa wao kama wadau wa kuu wa sekta ya bahari wamaandaa elimu kwa kufundisha vijana maswala yanayohusu bahari ili kila mmoja awe anajua kikamilifu dhana nzima ya uchumi wa buluu.
Aidha Dk Gulumo amesema hii ni mara yao ya tatu kuandaa kongamano kama hilo, wakianzia mwaka 2023 na kusisitiza kwa sasa wanahitaji utashi wa kisiasa kwani serikali zote mbili zimekuwa zikisisitiza ukuwajibwa wa uchumi wa buluu ili kutekeleza dhana nzima ya uchumi wa buluu.
Aidha amezitaja nchi ambazo mpaka sasa zimethibitisha kushiriki kongamano Hilo kuwa ni pamoja na ghana Kenya, Uganda , Korea ambazo zitashiriki mkutano huo.
Gulumo amezitaka sekta mbalimbali kushiriki kongamano hilo, zikiwemo wizara mbalimbali ambazo zinahusika moja kwa moja kwenye sekta ya uchumi wa buluu.
Amesema DMI kikishirikiana na chuo dada Cha Reginal Maritane University kilichopo nchini Ghana, hivyo kwa pamoja wamedhamiria kuunganisha nguvu ili kusogeza mbele dhana nzima ya uchumi wa buluu barani.
Aidha Dkt Gulumo ametaja kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ” Uinzi na usalama baharini”
Mkutano wa mwaka huu utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere ulipo jijini Dar es slSalaam.
Akizungumzia maswala ya usalama Gulumo amesema jambo la usalama ni la kila mwananchi kwa kushirikiana kwa pamoja na serikali za nchi husika ambazo bahari umepita kwenye mataifa hayo.
Mbali na usalama Dkt, pia ametaja madhara mengine yanayoathiri uchumi wa buluu ikiwemo uharibifu wa mazingira ikiwemo shughuli mbali mbali za kibinaadamu.
Aidha amesema “tusipo kuwa na ulinzi na usalama wa baharini hatutoweza kufanya shughuli zetu ambazo zitatupelekea manufaa ya uchumi”
Katika hatua nyingine Dkt gulumo hakuacha kuzungumzia madhara ya uharibifu wa mazingira baharini ikiwemo kukosa mazao ya bahari ikiwemo samaki kutoweka na pia kuharibu hali ya asili ya mazingira ya baharini.
Pia ametoa wito kwa jamii kutokuharibu kuchafua vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa sababu kuharibu mazingira ya bahari.
Dkt Gulumo ametaja madhumnui makubwa ya kongamano hilo mwaka huu ni kutoa fursa kwa wadau wa uchumi wa buluu kukutana,kujadiliana, maswala yote na kubadirisha uzoefu ili kukuza uchumui wa buluu.