Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara afya imepokea vidonge vya matone ya Vitamini A milioni 22 kutoka kwa shirika la Nutritrion International kwa ajili ya kuwapatie watoto walio na umri chini ya miaka 5 wapatao milioni 11 kwa ajili ya kuongeza kinga ya mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto hao
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Machi 13, 2024 Mollel wakati wa makabidhiano ya vidonge vya matone ya Vitamini A kutoka shirika la Nutrition International NI jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mollel amesema Vidonge vya matone ya Vitamini A vitasaidia kuongeza kinga ya Mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto walio na umri chini ya miaka tano.
Amesema elimu ya mtoto inaanza siku mimba inatunga na sio shuleni kwa kumpatia Mama lishe iliyobora wakati wa ujauzito ili kusaidia kuimarisha ubongo wa Mtoto
“Wazazi zingatieni lishe bora kwa watoto tangu wa utangaji wa mimba na kuwa na desturi ya kula mlo bora kwa mama wajawazito na hii itamsaidia mtoto hata baada ya kuzaliwa na wakati yuko shule ubongo na akili yake kufanya kazi kikamilifu pia itamuepunga na magonjwa ya mara kwa mara” Dkt. Mollel
Dkt. Mollel amewataka Watanzania kuzingatia milo yao ya kila siku kwa kupata chakula chenye lishe hasa vyenye vitamini ili kuepugana na magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu , magonjwa ya moyo na kisukari
“hivi sasa watu wanakula kupitiliza na hawazingati chakula nyenye lishe ivyo na kupelekea watanzania kusumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama uzito uliopitiliza, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kisukari. Niwatake wahudumu wa afya ngazi ya jamii mkawape elimu watanzania waweze kutofautisha kati ya shibe na lishe” amesema Dkt. Mollel.
Ameongeza kuwa ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Tsh. bilioni 99 kwa ajili ya kuajiri na posho za wahudumu wa afya ngazi ya jamii pia wamekuwa msaada mkubwa wa kufikisha elimu ya lishe na afya bora kwa jamii
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho kikwete ambae pia ni mjumbe wa bodi ya menejimenti nchini ya shirika la Nutrition International (NI) amesema shirika la Nutrition Internation limepatia Serikali vidonge vya matone vya Vitamini A milioni 22 kwa mwaka 22 na kuongeza kuwa vitamini A umsaidia mtoto kuimarisha afya ya macho na kuongeza kinga mwinili.
“Shirika la NI imetoa vidonge vya matone ya Vitamini A milioni 22 zitakazotolewa kwa awamu 2 yaani mwezi Juni na Disemba kwa watoto takribani milioni 11 walio chini ya miaka 5 na faida ya vitamini hivi ni kuimarisha afya ya macho na kuongeza kinga ya mwili kwa mtoto hivyo ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha watoto wanapatiwa matone haya” amesema Jakaya.