Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia
Mwakilishi wa Tanzania wa Mashindano la Mrembo wa Dunia (Miss World 2024)Halima Kopwe amewaomba wadau mbalimbali kuwekeza kwenye tasnia ya urembo kama inavyofanya vilabu mpira ili vijana wengi kupenda tasnia hiyo na kuweza kuitangaza Tanzani Kimataifa.
Akizungumza Machi 13, 2024 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akizungungumzia kuhusu ishiriki wake kwenye mashindano hayo ambapo amebainisha kuwa hiyo ilikuwa ndoto yake tangu alipokuwa darasa la nne licha ya kupitia changamoto mbalimbali za kukatishwa tamaa na ndugu jamaa na marafiki lakini alisimama imara.
“Nchi yetu tunakila kitu maana hata nimeshiriki mashindano ya Miss World sijaona kitu kikubwa ambacho wenzangu walivyokuwa wanasaidiwa na nchi zao hivyo sisi kama nchi hatuwezi kufanya wenzetu wamewekeza sana unakuta mtu vazi la ubunifu anavalishwa na mbunifu mkubwa wa nchi husika tofauti na sisi mpaka utafute mwenye kwa gharama zako mimi naamini serikali ikiwekeza kwenye tasnia hii kama wanavyofanya kwenye mpira tutafika mbaliā amesema Kopwe.
Miss Halima amesema safari yake haikuwa rahisi Mungu alimuwezesha hadi ameweza kuiweka nchi kwenye rekodi nzuri baada ya kuingia kwenye kumi bora kupitia project yake ya Damu yangu kizazi changu yenye lengo la kumsadia mwanamke mjamzito na mtoto.
“Project yangu niyoibuni kwa kuweza kuigusa jamii moja kwa moja imeweza kuingia kwenye 10 bora lakini pia kurudisha ushindi wa kuingia kwenye 40 bora ambapo ushindi huo kama nchi uliupata mwaka 2005″amesema Miss Halima
Sambamba na hayo amewaomba wadau kumshika mkono apate kununua gari la kupelekea wagonjwa katika Mkoa wa Mtwara kupitia project hiyo kwani ipo chini taasisi ya miss Tanzania bado anahitaji kuendelea kuisaidia jamii yake kama sehemu ya maisha yake .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ukuzaji na maendeleo ya sanaa baraza la taifa la sanaa(BASATA) ameipongeza kamati ya Miss Tanzania kwa kuweza kumsimamia mrembo huyo mpaka kuletea nchi heshima hivyo wameahidi kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha tasnia ya urembo inaendelea kuiwakilisha nchi kwenye mataifa mengine.
Naye,Muwakilishi wa mkurugenzi wa kampuni ya The look Bi.Halima Mhando amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameitendea haki tasnia ya urembo na sanaa kwani hata mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia uwekezaji mkubwa anaoufanya lakini pia kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour ambayo imefanya nchi kujulikana