Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Serikali imetangaza kupungua kwa maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo matende na mabusha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza na waandishi hii leo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema nchi imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha inatokomeza magonjwa ya matende na busha kwa kuokoa watu milioni 31.2 waliokuwa na hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo.
Alizungumza na waandishi wa Habari, leo Machi 12,2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kutokimeza ugonjwa huo nchini hususani mkoa wa Dar es salaam.
Amesema awali maambumizi makubwa ya ugonjwa huo yalikuwa katika Halmashauri 119 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wameza kudhibiti ugonjwa huo katika Halmashauri 112 kati 119 na kubakiwa na Halmashauri 7.
Amesema katika Mkoa wa Dar es Salaam Halmashauri zote yaani ya Manispaa ya Kigamboni na Ubungo,Temeke na Halmashauri ya jiji hazina maambukizi mapya ya ugonjwa huo baada ya kusitisha umezeshaji wa kingatiba na kub