Na Jumanne Magazi, Jamhuriamedia, Dar es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk Dorothy Gwajima ametoa rai kwa taasisi mbalimbali nchini kuendelea kuwekeza kwa wanawake, kwani kwa kufanya hivyo, ni kuongeza kasi ya maendeleo, kukuza ustawi wa jamii, na kujenga familia bora kwa maslahi ya Taifa .
Wito huo ameutoa leo Machi 6,2024 jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuhitimisha mafunzo ya mwanamke kiongozi awamu ya tisa yaliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo yalilenga kuwajengea uwezo wanawake kumudu nafasi za juu za uongozi.
Amesema wanawake ndio msingi mkubwa wa maendeleo katika ngazi tofauti kuanzia familia hadi Taifa hivyo kuwekeza kwa mwanamke ni kuliendeleza Taifa.
Aidha Dk Gwajima amewataka wanawake ambao wamehitimu mafunzo hayo na wapo kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kuhakikisha wanawasaidia wanawake wengine.
“Wanawake tushiakamane,na ninyi mliopo maeneo ya kazi, muwanyanyue na wengine, muwasaidie ili na wao watimize malengo yao msiwe visababishi vya misongo ya mawazo.