Na Mwandishi wetu, JamhuriMedia, Dar wa Salaam
WATUMISHI wanawake kutoka Chama Cha Qafanyakazi (TUICO) wameugana na wenzao nchini kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Dunia Heri kilichopo Kigamboni Kimbiji.
Siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8, kwa mwaka huu inaogozwa na kauli mbiu ya ‘Wekeza kwa wanawake ongeza kasi ya Maendeleo’.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha msaada huo kwa uongozi wa kituo hicho , Mkuu wa Idala ya wanawake, Afya na usalama na watu wenye ulemavu TUICO, Witness Mwijage.
Amesema katika kuadhimisha siku ya wanawake wameguswa kutoa matendo ya huduma kwa watoto yatima wanaoishi katika kituo hicho.
“Wanawake kutoka TUICO tumeguswa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Dunia heri kwetu sisi haya ni matendo ya huduma “amesema Witness
Akitaja baadhi ya vitu ambavyo wametoa katika kituo hicho ni pamoja na Mchele, Unga, Sukari, Maji, sabuni , chumvi pamoja na vitu vingine mbalimbali.
Aidha aliiushukuru Uongozi wa mzima wa TUICO pamoja na wadau wengine ambao wameweza kuwaunga mkono na hatimaye kufika katika kituo cha Dunia Heri kutoa msaada.
Pia alitoa rai kwa wanawake wengine kuinga mfano wa wanawake hao wa kuwa na utaratibu wa kutoa matendo ya huduma kwa watu wenye mbalimbali wasiojiweza na yatima.
“Nitoe wito kwa wanawake wengine kuwa na utaratibu wa kuwatembelea watu wenye mahitaji maalumu kufanya hivi kunatoa faraja kwao ..pia sio mpaka tusubiri mpaka siku ya wanawake duniani bali hata wakati mwingine “amesema
Awali Msimamizi wa kituo kulelea wa yatima cha Dunia heri , Beata Kusel aliwashukuru wanawake wa TUICO kwa moyo waliouonesha na kuguswa na kuamua kufunga safari mpaka katika kituo hicho jwa lengo la kuwapatia vitu mbalimbali jambo ambalo limewapa faraja.
“Tumefurahi sana kupokea msaada huu kutoka kwa wanawake TUICO kwetu tumefarijika sana kwani mmeonesha moyo mzuri wa kuja kuwaona na kuwasaidia watoto hawa”amesema Beata.
Aidha amesema kituo hicho kinawatoto 37 huku watoto 15 wakiwa ni wanafunzi piawakitarajia kupokea watoto wengine saba kutoka kijijini.
Awali siku ya wanawake ilitambulishwa rasmi na Umoja wa Dunia mnamo 1977 baada ya kuibuka kwa mara ya kwanza kutoka katika shughuli za utekelezaji wa Karne ya 20 huko Amerika Kaskazini na Ulaya.