Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amemtaka Rais Joe Biden kuandaa mdahalo wa wao wawili kufuatia Trump kuonekana kupata ushindi katika kura za jumla za mchujo, maarufu kama Super Tuesday, zilizofanyika wiki hii.

Trump aliitisha mdahalo huo muda mfupi baada ya mpinzani wake, Nikki Haley, kujiondoa katika kinyang’anyirocha kuwania kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican katika uchaguzi wa Novemba.
Trump amesema ni muhimu kwa Marekani kwamba yeye na Biden wataachwa kujadili masuala muhimu kwa raia wa taifa hilo na kutaka mdahalo huo ufanyike wakati wowote na mahala kokote.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampeni ya rais Biden bado hajatoa tamko lolote juu ya ombi hilo la Trump.