Na Mwandishi Wetu
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi kilichotokea Februari 29,2024 jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu TASWA, Alfred Lucas imeeleza kuwa Rais Mwinyi alikuwa mdau wa michezo, ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za tuzo za wanamichezo bora Tanzania ‘Tuzo za TASWA’ za mwaka 2011 zilizofanyika Juni, 2012 ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
“Siku hiyo TASWA pia ilitoa Tuzo ya Heshima kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu ‘Taifa Stars’ waliocheza mechi za kufuzu fainali za mataifa huru ya Afrika zilizofanyika Nigeria mwaka 1980”.imeeleza taarifa hiyo.
Chama hicho kimetoa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan, familia ya Mwinyi, wanamichezo na Watanzania kwa ujumla kufuatia msiba huo, “tukiamini namna bora ya kumuenzi kwa wanamichezo ni kuhakikisha wanafanya vizuri kimataifa”.imeeleza taarifa hiyo.