Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo zilizopo Jijini Mbeya leo tarehe 22 Februari, 2024.

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuboresha maendeleo ya Mkoa huo ikiwemo Jiji la Mbeya katika sekta mbalimbali.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifurahi jambo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera wakati walipokutana katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo zilizopo Jijini Mbeya leo tarehe 22 Februari, 2024.

PICHA NA OFISI YA BUNGE