WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi imeingia makubaliano na wizara ya uchukuzi kutoka nchini Misri yenye nia ya kutengeneza kipande cha barabara inayopita katika mikoa 6 hapa nchini na inayoitwa inaitwa “The Cairo to Cape Town Trans Number 4” (Barabara kuu kutoka Cairo kwenda Cape Town Afrika Kusini) inayopita katika nchi za kaskazini ambayo inatajwa kuzidi kufungua uchumi wa Tanzania.
Barabara hiyo itahusisha mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Dodoma, Manyara na Arusha mpaka mpakani Namanga kuelekea nchini Kenya mpaka Cairo Misri.
Akizungumza waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa amesema kuwa mashirikiano hayo ambayo ni matokeo ya ushirikiano mwema baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiyaimarisha hali ambayo inazidi kuvutia wawekezaji wa mdani na nje ya Afrika katika sekta mbalimbali.
“Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kuendelea kuimarisha mahusiano na nchi mbalimbali, wenzetu kutoka Misri wakiongozwa na waziri wa miundombinu tumekutana nao sisi wizara ya ujenzi tumejadiliana kushirikiana kimkakati tunayo barabara ya kutoka Misri inapita nchi za kaskazini na kuja hapa nchini kwetu kwenda Zambia mpaka Afrika ya Kusini.
“Tumejadili ni namna gani tutashirikiana kuimarisha huu mtando wa barabara kuiunganisha Afrika , kipande hiki kwa upande wa nyanda za juu kusini hapa kwetu kinapita katika mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Dodoma, Manyara na Namanga kuelekea kule Cairo kwahiyo tumekubaliana kushirikiana kukarabati kwa viwango vya kisasa namna tulivyojadiliaana ni namna gani mtandao huu wa biashara utaunganisha Afrika ” alisema Bashungwa.
Amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kuimarisha uchumi wa nchi kupitia miundombinu bora huku wanafunzi wa wa kada ya uhandisi wakipata nafasi ya kwenda kujifunza kwa vitendo nchini Misri.
Kufuatia mradi huo waziri Bashungwa ametoa maelekezo kwa wakala wa Barabara Tanzania Tanroads kuhakikisha kuwa wanawatumia wahandisi vijana kila baada ya kilomita 20 lazima tuwe na wahandisi vijana lengo kubwa hasa ni kutekeleza maelekezo ya Rais kwamba kukua kwa nchi yetu lazima kuendane na kuwawezes watanzania sisi wenyewe.
“Tumeweka msisitizo mkubwa kwamba jambo hili lifanyike kwa haraka na barabara hii ikishatengenezwa kwa viwango vya kisasa vitasaidia sana kukuza uchumi wa nchi , lakini tumekubaliana wanafunzi wa uhandisi ambao watamaliza katika vyuo vyetu watakwenda kujifunza kwa vitendo nchini Misri na tutakuwa na mkutano ambao tumeita vijana wote wahandishi”
“Nimewaelekeza wakala wa barabara Tanroads kuhakikisha kuwa vigezo katika barabara mpya ambazo zitajengwa kunakuwa na vipengele vya kulazimisha wakandarasi kuwachukua vijana katika kusimamia miradi na katika hili tutaangalia ni kilomita ngapi za mradi kwa kila mkandarasi anazojenga achukie vijana wangapi na hapa lengo kubwa hasa ni kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba kukua kwa uchumi wa nchi yetu lazima kuendane sambamba na kuwawezesha watanzania kujenga uchumi sisi wenyewe” alisema Bashungwa.