Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar ea Salaam
Maofisa wa Jeshi la Polisi 155 waliopandishwa vyeo na Rais Samia Suluhu Hassan wamekula kiapo cha utii kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura.
Maofisa hao pia wamekula kiapo cha maadili ya viongozi wa umma na kuahidi kupanda kwao vyeo kutakuwa chachu ya mabadiliko ya kiutendaji.
Waliokula kiapo hicho jana Februari 19/2024 chini ya IGP Wambura ni makamishna wasaidizi waandamizi wa Polisi(SACP), 27 waliopanda vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Polisi.
Miongoni mwao ni SACP, David Misime, Ulrich Matei, Gustavus Babile, Robert Mayala. Wengine ni Lazaro Mambosasa, Renata Mzinga na Neema Mwanga.
Aidha maofisa wengine 128 wamekuwa makamishna wasaidizi wa Polisi waandamizi wa Polisi.
IGP Wambura amesema wananchi watarajie mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika Jeshi la Polisi.