Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Chama cha ACT Wazalendo Kimewashauri wanachama hai waliolipa ada ndani miezi 12 kijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Chama ngazi ya Taifa ambapo zoezi la kuchukua fomu ni kuanzia 14Februar ha 24 ,2024.
Akizungumza leo Februai 14, 2024 na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Taifa Jora Bashange amesema nafasi za kugombewa ni ikiwemo viongozi Wakuu wa Kitaifa,Wajumbe wa Halmashauri kuu , Kamati kuu, ngome ya wanawake Taifa, vijana, wazee, na kila atakayechukua fomu ahakikishe amelipia ada aje na anstakiwa kwenda na stakabadhi za benki.
Aidha, akitangaza nafasi mbalimbali zinazogombewa ndani ya chama hicho ni pamoja na viongozi wakuu wa kitaifa ambapo ni kiongozi wa chama, Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa Tanzania Bara pamoja na Makamu Mwenyekiti Taifa Tanzania Zanzibar huku wajumbe wa Halmashauri Kuu ikiwa ni nafasi 24 na ujumbe wa kamati Kuu ni nafasi 24.
“Kwa upande wa Ngome wanawake Taifa, ni nafasi ya Mwenyekiti wa ngome ya wanawake Taifa, Makamu Mwenyekiti, Ujumbe wa Halmashaur Kuu Taifa nafasi 2, Ujumbe Mkutano Mkuu Taifa nafasi 2, huku upande wa Ngome Vijana Taifa ni nafasi ya Mwenyekiti wa ngome ya vijana Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Ujumbe halmashauri Kuu Taifa nafasi 2 na Ujumbe wa Mkutano Mkuu nafasi 2” amesema Bashange.
Ameongeza kuwa, utaratibu wa kuchukua fomu na kurejeshwa itakua ni Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Magomeni Dar es Salaam, Vuga Zanzibar, Ofisi za mikoa na majimbo yote ya ACT Tanzania nzima huku watakao chukua fomu wakitakiwa kufika na stakabadhi ya malipo ambayo ni bank slip inayoonyesha wamefanya malipo kupitia akaunt ya Chama.
Hata hivyo, ameeleza kuwa wale wagombea wa Ngome ya vijana na wazee wanaporejesha fomu waambatanishe na nyaraka zinazoonesha uthibisho wa umri wao pamoja na picha 2 za passport size wakati wa kurejesha fomu.
Aidha, ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine kutakuwa na mdahalo wa watia nia wa uenyekiti Ngome ya vijana feb 20, Uenyekiti gome Wanawake feb 27 pamoja na wagombea wa nafasi ya kiongozi wa chama na Mwenyekiti wa chama Taifa na Makamu wenyeviti Bara na Zanzibar Machi 4, 2024.
Katika hatua nyingine wanachama wa chama hicho wamejitokeza kumchukulia fomu ya kugombea Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othmani Masoud Othmani na wanampelekea Zanzibari