●Serikali yawekeza Bil.157.8/-, Matokeo chanya yaanza kuonekana
●Yajivunia kuwa na tozo nafuu kuliko bandari shindani ukanda wa Afrika Mashariki
Na Stella Aron, JamhuriMedia, Mtwara
BANDARI ya Mtwara ni mojawapo kati ya bandari kuu tatu za mwambao wa bahari zilizopo nchini, zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) bandari nyingine ni Dar es Salaam na Tanga.Bandari hii inasimamia bandari za Lindi na Kilwa.
Bandari ya Mtwara ilijengwa miaKa 1950 ikiwa na uwezo wa kuhudumia tani 400,000 kwa mwaka kwenye gati lenye urefu wa mita 385 na kina cha mita 9.5 (chart datum).
Meneja wa Bandari ya Mtwara Ferdinand Nyathi anasema kuwa bandari kwa sasa ina uwezo wa kupokea meli zenye urefu wa hadi mita 230 na upana wa lango la kuingilia meli ni mita 250 na kina cha zaidi ya mita 20.
Nyath anasema kuwa kutokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari ya Mtwara ujenzi wa gati moja la nyongeza lenye kina cha mita 13 (chart datum) na urefu wa mita 300, Bandari ya Mtwara kwa sasa ina uwezo wa kuhudmia zaidi ya tani 1,000,000 kwa mwaka.
Bandari ya Mtwara inatumika katika kufanikisha biashara kwa bidhaa zitokanazo nchini kwenda nchi za nje ikiwamo Msumbiji, Comoro, India na Vietnam pia anaongeza kuwa bandari hiyo imekuwa ikihudumia zaidi shehena ya korosho ambayo ni zao kuu la biashara kwa mikoa ya Kusini.
“Bandari hii inahudumia pia shehena za saruji, bidhaa za vyakula, mitambo kwa ajili ya miradi mbalimbali pamoja na shehena ya majimaji ikiwamo kemikali na mafuta. Sambamba na huduma hizi pia imekuwa msimamizi wa bandari za Lindi na Kilwa,’’ anasema.
Nyath anasema kuwa Bandari ya Mtwara inarahisisha shughuli za kibiashara kwa mikoa ya Kusini mwa Tanzania na Zanzibar pamoja na nchi za Msumbiji, Comoro, India na Vietnam n.k.
Anongeza kuwa, bidhaaa kuu zinazopita bandari ya Mtwara ni pamoja na korosho ghafi, saruji, bidhaa za chakula, shehena ya miradi, mafuta, makaa ya mawe pamoja na mizigo mchanganyiko.
HALI YA UTENDAJIKAZI 2019- 2024
Nyath anasema kuwa shehena (tani) iliyohudumiwa katika bandari ya Mtwara kwa mwaka 2018-19 hadi 2023 -24 (Julai 23 hadi Januari 24) ambapo mwaka 2018-19 tani zilizopakuliwa ilikuwa ni 45,072 na zilizopakiliwa 61,098 na kufanya jumla ya tani zilizohudumiwa kuwa 106, 170.
Kwa mwaka 2019-20 tani zilizopakuliwa zilikuwa 30,433 na zilizopakiwa ilikuwa 243,034 hivyo kufanya jumla ya tani kwa mwaka huo zilizohudumiwa kuwa tani 273,467.
Mwaka 2020- 2021 tani zilizopakuliwa zilikuwa 42,225 na zilizopakiwa ni 135,163 hivyo kufanya jumla ya tani zilizohudumiwa kuwa 177, 388.
Pia kwa mwaka 2021-22 tani zilizopakuliwa zilikuwa ni 85,887 zilizopakiliwa 506,488 hivyo kufanya tani zilizohudumiwa kwa mwaka huo kuwa tani 592,365.
Kwa mwaka 2022- 23 tani zilizopakuliwa ilikuwa ni 92,190 na zilizopakiwa zilikuwa ni 1,536,485 hivyo kufanya jumla ya tani zilizpohumiwa kwa kipindi hichio kuwa ni 1,628,615.
Julai 23 hadi Januari 2024 jumla ya tani zilizopakuliwa kuwa ni 115, 141 na zilizopakiwa kuwa 901,155 hivyo kufanya jumla ya tani zilizohumiwa kwa kipindi cha Julai 23, 2023 hadi Januari 2024 kuwa tani 1,016, 296.
“Kwa mchanganuo huo utaona kuwa utendajikazi wa bandari umekuwa ukikua kila mwaka kutokana na kuwepo kwa uboreshaji uliofanywa na Serikali hivyo umechangia pia idadi ya watumiaji wa bandari ya Mtwara kuongezeka kwani wanapata huduma bora na kwa wakati,” anasema.
Na kwa upande wa kimataifa kutokana na uboreshaji uliofanywa na Serikali, meneja huyo amesema kuwa kumekuwa na mafanikio na kwa kipindi cha 2018-19 hadi 2023-24 (Julai 2023 hadi Januari 2024.
“Kwa mwaka 2018- 19, kimataifa meli zilizohumiwa zilikuwa 16 na kwa mwambao meli zilikuwa 125 na kufanya idadi ya meli zilizohudumiwa kuwa 141. Kwa mwaka 2019- 2020 kimataifa meli zilizohduumiwa zilikuwa 32 na mwambao 78 na jumla kuwa 110.
“Mwaka 2020- 21 kimatifa meli zilizohudumiwa zilikuwa 26 na mwambao meli zilikuwa 58 jumla kufanya meli zilizohudumiwa kuwa 84. Mwaka 2021- 2022 kimataifa meli zilizohumiwa zilikuwa 50 na mwambao 116 jumla meli zilizohudumiwa ni 166.
“Mwaka 2022- 23 kimataifa meli zilizohudumiwa zilikuwa 106 na mwaka zilikuwa 207 na jumla kuwa 313. Pia kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Januari 2024 kimataifa meli zilizohudumiwa zilikuwa 94 na mwambao ni meli 93 na kufanya meli zilizohudumiwa kuwa 187,” anasema.
SHEHENA YA MAKASHA YALIYOHUDMIWA
Meneje huyo amezungumzia shehena ya makasha yaliyohudumiwa katika Bandari ya Mtwara kwa kipindi cha 2018- 19 na Julai 2023 hadi Januari 2024 na kueleza kuwa kulikuwa na mafanikio.
“Mwaka 2018 -2019 makasha yaliyopakuliwa yalikuwa 2,014 na yaliyopakiliwa yalikuwa 2,032 jumla yaliyohudumiwa kuwa 4,046.
“Mwaka 2019- 20 makasha yaliyopakuliwa ni 1,879 na yaliyopakiwa yalikuwa 1,822 jumla kuwa ni 3,701 na kwa mwaka 2020 -21 makasha yaliyopakuliwa yalikuwa 90 na hakukuwa yaliyopakiwa na kufanya jumla kuwa 90 ambapo kwa mwaka 2020-2021 hakukua na shehena ya makasha yaliyopakiwa.
“Kwa kipindi cha mwaka 2022-23 makasha yaliyopakuliwa 3,678 na yaliyopakiwa yalikuwa 2,401 na kufanya jumla ya makasha yaliyohudumiwa kuwa 6,079.
Julai 2023-Januari 2024 makasha yaliyopakuliwa yalikuwa 19, 990 na yaliyopakiwa yalikuwa 18,465 hivyo kufanya jumla ya makasha kwa kipindi hicho yaliyohudumiwa kuwa 38,455.
MIUNDOMBINU YA BANDARI
Katika kuhakikisha kuwa bandari ya Mtwara inafanya vizuri, Serikali imewekeza katika eneo hilo na kuchangia kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya utendajikazi na hata kuwepo jambo ambalo limesaidia kuwepo kwa maendeleo.
Meneja wa bandari hiyo anasema kuwa geti ya zamani lina kina cha mita 9.5 (CD), Urefu wa mita 385 na uwezo wa kuhudumia hadi tani 45,000DWT.
YADI GATI ZA ZAMANI
Meneja huyo anaongeza kuwa kuna yadi tatu zenye ukubwa wa mita za mraba 38,000 na uwezo wa kuhifadhi makasha 4,350 (TEUs) kwa wakati mmoja.
“Uwepo wa yadi hizi unasaidia uhifadhi wa makasha kwa wingi hivyo ni jambo la kuishuruku Serikali kwa namna ambavyo imeongeza nguvu kwenye uwekezaji bandari nchini,’ anasema.
GETI JIPYA
Kina cha mita 13.0 (CD), urefu wa mita 300 na uwezo wa kuhudumia hadi tani 65,000 (DWT). Ujenzi wake uligharibu shilingi bilioni 157.8.
YADI KATIKA GATI JIPYA
Anaongeza kuwa yadi yenye ukubwa wa mita za mraba 75,808 ina uwezo wa kuhifadhi makasha 8,600 TEUs kwa wakati mmoja ambapo ni yadi katika geti jipya.
Anasema kuwa SSG TPA imepokea crane ya kisasa iitwayo Ship two shore gantry crane (SSG) mtambo huu umeshasimikwa katika bandari ya mtwara na wenye uwezo wa kuhudumia makasha 25 (TEUs) kwa saa.
SCNAER
Anaongeza kuwa Scaner moja ambayo inaweza ‘scane’ hadi makasha 30 kwa saa.
Bandari ina maghala mawili ya kuhifadhi mizigo (Zambia shed na Shen no. 3) yenye ukubwa wa mita za mraba 12,5000 na uwezo wa kuhifadhi tani 18,000 za mizigo kwa wakati mmoja.
“Vifaa vya kuhudumia mizigo vilivyoboreshwa ambapo kuna reach stackers tatu zenye uwezo wa kubeba tani 45 na kuna mashine tano za kubeba makasha matupu zenye uwezo wa kubeba tani 8 hadi 12, mbali ya vifaa hivyo pia kuna fork lift 13 zenye uwezo wa kubeba tani 3 hadi 42.
“Pia kumefanyika uboreshaji mwingine kwa kuongeza mobile crane tatu zenye uwezo wa kubeba tani 30 hadi 50 pia kuna wheel loaders mbili,” anasema.
Anaongeza kuwa kuna vyombo vya kuhudumia meli kama two berthing tungs, one mooring boat, boti moja ya mapilot na zingine boti tatu za kufanya ukaguzi.
SIFA ZA KIPEKEE BANDARI YA MTWARA
Bandari ya Mtwara ina jumla ya hekta 2,712 za ardhi ambayo zinaweza kutumika kwa upanuzi na uendelezaji wa bandari. Kituo kilichopo – 70 H.a, Kisiwa Mgao – 25 H.a, Msangamkuu na Ng’wale 2,623 H.a pia bandari ina mizani sita.
KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA (FLOW METER)
Bandari ina mita za kupimia mafuta ili kuweza kujiridhisha kiwango cha mafuta kinachoshuka melini.
MIFUMO YA TEHAMA
Anasema kuwa Bandariya Mtwara ina mifumo ya baharini, mizigo na malipo kwa ajili ya kushughulikia kila aina ya mzigo ambapo bandari inafanyakazi kwa saa 24.
Pia bandari ya Mtwara inazingatia viwango vya kitaifa na kimataifa kituo hiki kinatii kanunu za ISPS na kinatii zaidi mahitaji yote ya udhibiti wa ndani na kimataifa.
PUNGUZO LA TOZ0
Bandari ya Mtwara hutoza tozo ya Wharf kwa asilimia 0.5 kwa mizigo ya makasha ya makaa(containerized cargo) inayosafirishwa au kupokewa (export and import) – Bandari nyingine hutozwa Wharfage kwa asilimia 1.
Meneja anasema kuwa tozo katika bandari ya Mtwara ni nafuu kuliko bandari shindani ukanda wa Afrika Mashariki.
‘Kwa mfano, wakati bandari nyingine zikitoza tozo ya ‘wharfage’ kwa asilimia moja, sisi tozo hiyo ni asilimia 0.5 tu kwa mizigo ya makasha inayosafirishwa shindani ukanda wa Afrika Mashariki.
Kwa mfano, wakati bandari nyingine zikitoza tozo ya ‘wharfage’ kwa asilimia moja, sisi tozo hiyo ni asilimia 0.5 tu kwa mizigo ya makasha inayosafirishwa au kupokewa.”
Anaongeza kuwa TPA pia imepunguza tozo ya ‘shore handling’ na ‘stevedoring’ kwa asilimia 30 kwa Bandari ya Mtwara.
“Punguzo halitokani na hofu, bali ni mikakati ya kibiashara na masoko.,Ifahamike kwamba shehena kubwa ya saruji ya Dangote kwenda visiwa vya Comoro na Zanzibar inapita hapa.”
Anasema Mtwara ni bandari ya kimkakati, ikilenga kuhudumia ushoroba wa kusini kutoka pwani ya Bahari ya Hindi hadi Mbamba Bay,pwani ya Ziwa Nyasa.
“Lengo la serikali ni kuifungua kusini. Sasa inaifunguaje? Ni kwa kujenga bandari, barabara na reli. “Sisi (TPA) tupo hatua kadhaa mbele kwa kuwa maboresho ya Bandari ya Mtwara yanaendelea huku Waziri Mbarawa (Profesa Makame Mbarawa,
Waziri wa Uchukuzi) akiwa tayari amesaini mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay. “Barabara tayari ipo na inatumika na ninaamini kuwa mikakati ya ujenzi wa reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay inaendelea vema.
“Haya (upanuzi wa Bandari ya Mtwara, ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay, barabara na reli) yakikamilika, Mtwara itabadilika na ufanisi wa bandari utakuwa ni wa hali ya juu
zaidi,” anasema .
Mbali na Zanzibar na Comoro, Bandari ya Mtwara inarahisisha shughuli za kibiashara kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania, Msumbiji,Comoro, India na Vietnam.
“Wafanyabiashara wanapaswa kufahamu kwamba kutumia Bandari ya Mtwara ni nafuu zaidi kuliko bandari shindani,” anasema .
Mbali na saruji, bidhaa kuu zinazopita Bandari ya Mtwara ni korosho ghafi, bidhaa za chakula, shehena ya miradi, mafuta, makaa ya mawe na mizigo mchanganyiko.
Anatoa rai kwa serikali akiiomba iendelee kutekeleza mipango yake katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa nchi kavu hasa reli, ili kuchochea matumizi ya Bandari ya Mtwara kwa kuiunganisha na maeneo mbalimbali.
Kujengwa kwa reli kutarahisisha usafirishaji wa shehena za madini ya chuma na makaa ya mawe kutoka bara mhadi Mtwara pamoja na mazao ya chakula na biashara.
Pia kukamilika kwa Bandari ya Mbamba Bay na reli kutarahisisha usafirishaji wa shehena si za mikoa ya kusini pekee, bali hata nchi jirani za Malawi na Zambia.
Kwa upande wake, Nyati, anasisitiza akisema: “Ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa Bandari ya Mtwara ni wa hali ya juu sana.
Mamlaka inapunguza tozo ya shore handling na stevedoring kwa asilimia 30 kwa bandari ya Mtwara ukilinganisha na badari nyingine ambazo hutoza asilimia 100.
SRORAGE (MUDA WA KUHIFADHI MAKASHA)
Anaongeza kuwa Bandari ya Mtwara imeongeza muda wa kuhifadhi makasha matupu (empty cointer) kutoka siku 15 hadi 21 pia huongeza muda wa kuhifadhi makasha yenye mzigo (full caontiners) kutoka siku 7 hadi 14.
“Kwa hatua hiyo tumemrahisishia mfanyabiashara kupata muda mrefu wa kutoa mzigo wake bandarini bila kutoka gharama za nyongeza haya ni mafanikio makubwa katika bandayetu ambapo huduma tunazotoa katika bandari hii ni tofauto na zingine,” anasema.
FURSA ZILIZOPO
Meneja anasema kuwa kuna fursa mbalimbali ambazo hupatikana kama kilimo cha mazao mbalimbali yanayozalishwa katika Mkoa wa Mtwara na mikoa ya jirani ya Lindi na Ruvuma.
Shughuli za utafutaji wa mafuta, gesi uzalishaji wa gesi asili na bidhaa zitokanazo na gesi. Ujenzi wa miradi ya miundombinu na viwanda inayotarajiwa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma,
Uwepo wa bidhaa za madini na viwandani mbalimbali kati,ka ukanda wa maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor) na nchi jirani za Msumbiji, Malawi na Zambia.
CHANGAMOTO
Meneja anaongeza kuwa mbali ya mafanikio makubwa, bado kuna changamoto ya ukosefu wa miundombinu ya usafirishaji wa ardhini kama reli ambayo ingekuwa ni kiunganishi kutoka maeneo ya uzalishahi kama migodini ( Mbamba bay, Mchucuma na Liganga).
“Ukosefu wa meli za mwambao za uhakika ambazo zingesaidia kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka Mtwara kwenda Tanga na Dar es Salaam na nchi jirani ya Comoro hata hivyo tunaamini suala hili litapatiwa ufumbuzi na Serikali,” anasema.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), imedhamiria kuboresha utendaji wa bandari ya Mtwara ili iweze kuhudumia nchi za jirani za Comorom, Malawi, Msumbiji na Zambia pamoja na mikoa ya ukanda wa kusini mwa Tanzania ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ili kunufaika na fursa kubwa zilizopo.
“Rai yetu kwa Serikali ni kuomba iendelee kutekeleza mipango yake katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa nchi kavu hasa reli, ili kuchochea matumizi ya bandari ya Mtwara kwa kuiunganisha na maeneo mbalimbali,” anasema.