Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 – 2008 Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kilichotokea leo 10 Februari 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipokuwa akipata matibabu.
Mhe. Lowassa alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mapafu na shinikizo la damu hadi alipofariki dunia.
Marehemu Edward Ngoyai Lowassa amelitumikia taifa la Tanzania katika nyadhifa mbalimbali wakati wa uhai wake, amewahi kuwa Waziri wa Maji na Mifugo mwaka 2000 hadi 2005 na baadae kuwa Waziri Mkuu mwaka 2005 – 2008.
Rais Dk. Mwinyi anaitakia familia ya marehemu Lowassa, ndugu na marafiki moyo wa Subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Rais Dk. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi,