Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia, Dar ea Salaam
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalumu imesema inakwenda kuweka Mkakati Madhubuti ikiwemo kufanya mapitio ya sheria na kanuni itakayokwenda kusaidia kudhibiti Ukatili wa watoto Mtandaoni.
Ameyasema hayo leo Februari 9, 2024 Jijini Dar es salaam Waziri Wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalumu Dkt Dorothy Gwajima wakati akifungua Semina ya Usalama wa Mtoto Mtandaoni kwa Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari ambapo amesema Wazazi , amesema Teknolojia inakwenda kwa kasi na na maudhui yanayosambaa mtandaoni ni hatari kwa watoto hivyo Elimu haina budi kutolewa kwa walezi kwani wamejisahau na kuwapa watoto hao vifaa vya kielektroniki ikiwemo simu Tv pasipo kuwa karibu nao kujua nini wanakitazama watoto wameshaharubuniwa kupitia mtandao .
Samba na hayo taafiti uliyofanywa mwaka 2022 kwa watoto wa Tanzania watoto umri wa miaka 12 hadi 17 ulibainisha kwamba asilimia 67 ya watoto wanaotumia mitandao maarufu inayotumiwa na watoto ni pamoja na
Facebook, Twitter (X), Instagram, Whatsap, Tiktok na Telegram na utafiti
huo, asilimia 4 ya watoto waliotumia mitandao walifanyiwa aina tofauti za
ukatili kwenye mitandao ikiwa pamoja na kukutana na wahalifu waliwasiliana nao kupitia mitandao na asilimia 5 ya watoto waliotumia walishawishiwa au kulazimishwa kwa vitisho kutuma picha zao za utupu pamoja na faida nyingi za mitandao, athari zinazowakuta watoto katika hivyo atumizi ya mitandao bila uangalizi wa karibu zinajumuisha kuanza ngono katika umri mdogo hivyo kupata athari za kisaikolojia na mmonyoko wa maadili hivyo kusababisha mwingiliano wa mila na desturi za mataifa mengine ikiwa kuiga ushoga na usagaji.
“Tunakwenda kutoa muarobaini Kumekuwepo na jitihada mbalimbali za kisera na kisheria za Kimataifa, Kikanda na Kitaifa katika kuwalinda watoto na Vijana Balehe dhidi ya ukatili wa Mitandaoni zikiwemo Sheria ya Makosa ya Kujamiiana Na. 4 ya 1998 kifungu cha 12, Aidha, Vifungu vya 12 na 13 vya Kanuni za Maudhui mitandaoni, 2018 chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya
- Kifungu cha 13 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao, ya 2015 na Vifungu
vya 83 na 158 (1) na (b) vya Sheria ya Mtoto Na.21, 2009.” amesema Waziri tatizo hili kwa kutoa elimu na uelewa kuhusu Ukatili wa Mtoto mtandaoni namna ya kujilinda pia tutafanya mapitio ya sheria na kanuni na kusogea kwenye teknolojia ili mtoto anapotumia vifaa vya teknolojia anakuwa salama na hadhuriki na chochote ili tutengeneze kizazi kilicho bora na salama kinachotegemewa miaka ya usoni” amesema Waziri
Sambamba na hayo amesisitiza kuwa lazima Maudhui yasiyofaa yasimfikoie mtoto kwani Wazazi na Walezi lazima wawe kipaumbele kutimiza wajibu wa kufuatilia vifaa vya kiektroniki kwa watoto wao wanavyovitumia kwa kuwaawekea muda maalumu kutumia vifaa hivyo kwani wengine hawalali na vhuleshao usiku kucha wakichati na kupelekea kuona maudhui yasiyofaa na wengine kukataa shule bado wadogo na kuanza kujiingiza katika makundi ya matandaoni yasoyofaa pasipo mzazi kujua hivyo umakini unatakiwa sana hasa kwa kundi hilo .
Kwa upande wake Yusuphu Kileo Mtaalamu wa Masuala ya Mtandao na Uchunguzi wa makosa ya kidigitali amesema Dunia ilivyo sasa mtoto mdogo wa miaka anaweza kuiwasha simu akatafuta kile anachokihitaji ikiwemo katuni hivyo baadhi ya nchi ilipogundua hilo zimeanza kuchukua hatua na Tanzania hatujabaki nyuma na sisi mikakati inaanza mapema kwa kuanza na kuongezewa nguvu Sheria na taratibu kwani haizuiwi mtoto kutumia teknolojia lakini lazima Elimu itolewe kuwa na matumizi sahihi ya mitandao
Sanjari na hayo amesema kumekuwa na tabia ya Wazazi kuwapa watoto simu pasipo kujua nini wanachokizatama mtandaoni hivyo amesema kabla ya Mtoto kupatiwa simu apatiwe elimu kwani wengine hutumia kutuma.picha na kuandika jumbe pasipo kujua kesho yake inaweza kuwaathiri hivyo sasa Wazazi walezi tambueni kuwa teknolojia ni nzuri lakini je wako anachokitazama kinaendana na yeye .
” Mzazi Mlezi hakikisha Usimwachie Mtoto wako kifaa cha kielektroniki kama hujui nini anachokitazama bora umnyang’anye kwani utakuwa unamsaidia sana atasoma vizuri hadi pale atakapopata kabla ya kumpatia simu mpatie elimu kwanza na kuwa karibu naye anachokitazama kwani kuna wengine walikurupuka na sasa wanajutia kuko⁹
Aidha Februari 10 inatarajiwa kuafanyika tukio kubwa Dodoma la Uzinduzi wa kampeni usalama wa Mtoto Mtandaoni na uzinduzi wa Kamati ya ushauri ya Taifa ya Usalama wa Watoto Mtandaoni itakakayoongoza kampeni hizo ni “Usalama wa Mtoto Mtandaoni ni Jukumu letu Chukua hatua”.