Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dodoma
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imekamilisha kuingiza vituo vyote kwenye mfumo wa kuhifadhi taarifa zote za vituo kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa ili kuufanyia majaribio na pia kutazama gharama za usafirishaji dawa kupitia mfumo huo wa ndege maalum (drones) ukilinganisha na usafirishaji kwa njia ya magari ili maamuzi sahihi yafanyike.
Dkt. Mollel amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 83 kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ambapo swali hilo limeulizwa na Mbunge wa Kilindi Mhe. Omari Mohamed Kigua aliyeuliza “Je, ni lini Serikali itatumia Drones kusambaza Dawa katika Zahanati zetu Vijijini.”
Dkt. Mollel Amesema kuwa Serikali ilishakamikisha mfumo ambao unahifadhi taarifa zote za vituo kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa, Mfumo huu utasaidia kupata taarifa za kijiografia (Geo coordinates) za vituo vyote nchini.