Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar ea Salaam
TANROAD imefanya jitihada za haraka kurejesha mawasiliano barabara ya Kunduchi Mtongani ndani ya masaa 48 baada ya daraja la Tegeta kingo zake kubomoka kutokana mvua kubwa iliyonyesha Jumamosi kuamkia Jumapili na kusababisha magari kushindwa kupita kuelekea Ununio.
Akizungumza leo Januari 22, 2024 jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Ujenzi Godiphrey Kasekenya alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na mvua iliyonyesha Januari 20 ,2024 ikiwemo Jangwani na Mto Tegeta ambao unaendelea na ujenzi ambapo amesema Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitoa utabiri kuwa mwaka huu kutakuwa na mvua kubwa hivyo tumeshuhudia madhara makubwa ikiwemo kuharibika kwa miundombinu kama barabara , madaraja nyumba kubomoka.
“Kadhia hii iliyotokea kutokana na mvua nyingi karibua mikoa mingi imeathirika hivyo TANROAD imekuwa na ikipata tu taarifa ya uharibifu wowote kukabiliana na changamoto hii haraka kurejesha mawasiliano.
“Kwani walitoa taarifa kuwa baada ya masaa 48 watarejesha mawasiliano na wameshafungua barabara moja na wanajitahidi kufungua barabara hivyo Serikali nayo imekuwa makini sana kuhakikisha madhara yapotokea tu jitihada za haraka na makusudi zinachukuliwa kusaidia kurekebisha miundombinu yake.” amesema Waziri.
Naibu Waziri Kasekenya amewaagiza Tanroad wafungue njia zote mbili kwa juhudi kubwa kwani barabara zote ni za muhimu na Serikali ya Awamu ya Sita iko macho kukabiliana na majanga ya dharura na yasiyo na dharura kwa kufanya kazi usiku na mchana wananchi wanatakiwa wafanye shughuli zao za kiuchumi bila kero yeyote.
Eneo la daraja la Tegeta liko tayari limetengenezwa na linaendelea kuwekwa mawe makubwa ili kupitika kwa urahisi na Jangwani nimeona wanaendelea kuzoa tope ili magari yapite kwa urahisi na shughuli ishukuriwe ushirikiano uliotolewa na Kiwanda cha saruji Wazo Hill na Jeshi la Magereza.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha matengezeo TANROAD Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Suzan Lukasi amesema walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi madaraja yaliyoharibika kutokana na maji kubadili mwelekeo na hivyo kazi ilifanyika kwa kushirikiana na Wakandarasi wa dharura .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amewapa pole wale wote walipoteza ndugu zao katika hizo pia amewataka wananchi kuachana na kutupa taka ngumu katika mifereji ya maji .