- Dar es Salaam ni mji wa kibiashara hivyo ugonjwa wa Kipindupindu hautakiwi kupenyeza kabisa
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amepiga marufuku uzagaaji wa watu kwenye maeneo yote ya msingi kama vile Tanzanite bridge na Ubungo, watoto wa mitaani na ombaomba barabarani ambapo amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuwafukuza na wengine kuwakamata
Ameyasema hayo katika mkutano wake na Watendaji wa Serikali uliofanyika jijini humo uliohusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
RC Chalamila amesema Serikali imewekeza zaidi ya Tirioni 3 kwenye vituo vingi vya kulelea walemavu nchini ambapo Dar es Salaam kuna kituo kikubwa cha kulelea walemavu pia.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa imebainika kuwa ulemavu kwa sasa ni mtaji ambapo wale ambao sio walemavu huenda kuwakusanya walemavu Kisha kuwatembeza kwenye baiskeli ambapo jioni huchukua kilichokusanywa na walemavu hao na kuwapatia walemavu hao kiasi kidogo Cha pesa kati ya sh 3000 mpaka 5000 kwa siku
Kuhusu kamata kamata ya magari ya takataka RC Chalamila ameitisha kikao kati yake na Mwenyekiti wa wakandarasi, kundi dogo la wakandarasi, ZPC, ZTO ili baada ya Kikao hicho yatolewe maelekezo ya pamoja yatakayosaidia magari hayo kwenda kwa haraka
Dar es Salaam ni Mji wa kibiashara hivyo igonjwa wa kipindupindu hautakiwi kupenyeza kabisa na ndio maana amewaita wadau kusaidia upatikanaji wa vifaa vya Usafi, Wakuu wa Wilaya kuhakikisha Watendaji wanasimamia usafi kufanyika kila wiki, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi kuhakikisha uchafu haukai sehemu muda mrefu, Ras na Wakuu wa Wilaya kuendesha dampo kwa ubia na ulipaji wa ushuru bila shuruti.
Kwa upande wao, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wakili kupokea maagizo yote na kuahidi kuyafanyia kazi
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohamed Mang’ una ameeleza Nini kifanyike ili kudhibiti ugonjwa huo kuwa ni:-Halmashauri kutoa elimu endelevu ya kanuni Bora za Afya katika ngazi zote
Dawasa kuendelea kutibu maji yanatumiwa na jamii, Uondoshwaji wa taka ufanyike kwa wakati, Kuepuka ulaji wa vyakula vilivyoandaliwa katika mazingira machafu, wananchi kuchemsha maji, wananchi kuizingatia Usafi na usafi wa mazingira, kula chakula Cha Moto, vyakula vilivyopikwa vihifadhiwe vizuri, kuosha matunda kwa maji Safi na salama.
Ikumbukwe kuwa RC Chalamila atagawa Vifaa vya usafi Januari 20 na 21, 2024 kwenye vyombo vya dola