Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,imemteua Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM ambaye ameshika nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo aliyejiuzuru nafasi hiyo Novemba mwaka jana.
Kamati Kuu imemteua Emmanuel Nchimbi leo mjini Unguja , Zanzibar wakati wa kikao chake cha kawaida katika kujadili mambo mbalimbali ya chama chao.D
Dk Nchimbi sio jina geni katika masikio ya Watanzania hususani katika nyanja ya siasa kwani tayari ameshika nafasi mbalimbali katika Serikali zilizopita.