Mwanafunzi mmoja amewapiga risasi watu sita, na kuuwa mmoja katika shule ya sekondari katika jimbo la Iowa nchini Marekani na kisha kujitoa uhai.
Tukio hilo limetokea siku ya kwanza wanafunzi waliporudi shule baada ya mapumziko ya likizo, Polisi wamesema.
Watano kati ya waliopigwa risasi walikuwa ni wanafunzi na mmoja ni msimamizi wa shule.
Mwanafunzi aliyefariki alikuwa darasa la sita, ambalo ni la watoto wa miaka 11 au 12.
Mshukiwa huyo baadaye alitambuliwa kama Dylan Butler, alikuwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.