Na Abel Paul, Jeshi la Polisi- Arusha
Jeshi la Polisi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema katika kuhakikisha linakwenda na mifumo ya kisasa na mabadiliko ya kitekinolojia ikizingatiwa mji huo ni kitovu cha utalii hapa nchini huku mkoa huo ukipokea wageni wengi kutoka ndani ya nchi na mataifa mengine ambapo umeamua kuja na mfumo mpya wa ulinzi kwa kutumia Tehama.
Akitoa taarifa hiyo wakati alipotembelea kituo cha mawasiliano cha jeshi hilo mkoani humo Kamanda wa Polisi Mkoani hapo Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha halijabaki nyuma katika mabadilko ya teknolojia huku akibainisha kuwa limeimarisha ulinzi katika mkoa huo kwa kutumia mifumo ya kisasa ambayo itabaini moja kwa moja wahalifu wanaotenda makosa ndani mkoa huo.
ACP Masemajo amesema kuwa Jiji la Arusha ni miongoni mwa majaiji bora ambapo amebainisha kuwa jeshi hilo limeona vyema kwendana na hadhi ya jiji hilo ambalo ni lango la utalii nchini kwa kuboresha mifumo ya ulinzi wa kisasa akiwataka wananchi kutumia fursa hiyo ili kudhibiti uhalifu katika Mkoa huo.