Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA), ambapo imefanikiwa kukamata kg 3,182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni maalum iliyofanyika Jijini Dsm
RC Chalamila amesema pongezi nyingi zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uteuzi Mzuri wa Kamishna Jenerali Aretas Lyimo wa Mamlaka hiyo ambaye kwa kushirikiana na timu yake kuonyesha uzalendo na weledi Mkubwa Kudhibiti biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya Nchini
Aidha, Mkuu wa Mkoa amekiri kuwa DSM ndio lango la kuingizia na kuzisafirisha dawa hizo haramu ambapo husambaa nchi nzima hivyo ametaka vijiwe vyote vinavyofanya biashara hii harumu kukomeshwa Mara moja
Wakati huo huo RC Chalamila amesema kikosi kazi tayari kimeundwa ili kupambana na biashara hiyo haramu sambamba na kuwakamata wakwepa Kodi na vibaka
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lymo amesema oparesheni hii ni endelevu na kila atakayejihusisha na biashara hii haramu atakamatwa na Sheria itachukua mkondo wake
Hata hivyo, Kamanda wa Kanda maalum ya kipolisi Dsm Afande Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi litahakikisha linakata mashina yote na kuyamaliza madawa hayo haramu kabisa.