Waandishi wa habari wametakiwa kumsaidia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Samia Suluhu Hasan juu ya fedha anazozitoa kwaajili ya miradi.
Hayo ameyasema Mwenyekiti mstafu wa CCM Mkoa wa Mara Samweli Keboye alipokuwa akizungumza na waamdishi wa habari.
Keboye amesema Rais anatoka fedha nyingi za miradi lakini nyingine hazitumiki ipasavyo hivyo waandishi wa habari wanatakiwa kumsaidia sana kwaajili ya kufatilia utekelezaji wake.
Amesema fedha za miradi zinapokuja wananchi wahajui ni kiasi gani kupitia qaandishi wa habari wanatakiwa kujua mfano barabara,visima,madaraja imetumika shilingi ngapi kutekeleza miradi hiyo.
Akiendelea kuzungumza amewataka waandishi wa habari kuelekea uchaguzi wajiepushe kuandika habari za upendeleo badala yake wawe na uwiano kwani hali hiyo imepelekea baadhi ya Waandishi kufanya kazi hawako salama na kuchukiwa.
Amesisitiza kuwa waandishi wanaweza kuiweka nchi pazuri au pabaya lakini wanatakiwa kuhakikisha Inchi inakuwa na amani kwa kuandika mazuri ya Nchi ipasavyo kwa uwazi .
” Ukiona kiongozi hataki kushirikiana na Waamdishi wa Habari huyo si kiongozi mzuri ukiona kiongozi anabagua Waandishi wa Habari huyo sio kiongozi mzuri mimi kwenye uongozi wangu nilitumia sana waandishi wa habari hata mimi nikifanya makosa msiniache ” amesema Keboye.
Hata hivyo amewataka waamdishi wa habari kumpenda na kuthaminiana kama watoto wa baba mmoja na kuepuka majungu baadala yake wawe wamoja.