Na Mary Margwe, JamhuriMedia,Hanan’g
Jumla ya makamanda wapatao 1267 wanaendelea na shughuli mbalimbali katika eneo la wahanga wa maporomoko ya udongo yaliyotokea Novemba 3,2023 huko wilayani Hanang, ambapo kufuatia zoezi linaloendelea wamefanikiwa kuipata miili mingine miwili na kuweka jumla ya idadi ya vifo 65.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 5,2023 na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa wakati alipokua akizungumza na wananchi wa Kata mbalimbali Wilayani Hanang, ambapo Waziri Mkuu amesema misaada yote itakayotolewa watatumia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kwa upande wa wenyeji Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Kabla ya kufika Hanang Waziri Mkuu aliwatembelea kuwajulia hali majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara, pamoja na kuwatembelea wale waliokosa !ahali pa kuishi ambao wako kwenye makambi mashuleni.
” Tumetoka hospitali ya Babati kuwaona majeruhi pia tumewatembelea kambi ya walioathirika na maafa haya ambao wamepotelewa na nyumba wako salama katika vituo vitatu, wanaendelea kuhudumiwa, watakaa hapo huku timu kubwa ikiendelea ikiratibu maisha yao, tunaendelea kufanya tathimini ya athari na maeneo zingine kuonaathari zilizojitokeza ni kubwa kwa kiasi gani” amesema Waziri Mkuu.
” Miili yote imetambuliwa na ndugu zao na wanasindikizwa wafiwa na miili majumbani mwao ili familia ziendelee na taratibu kidini na kimila,hivyo tunatarajia hadi jioni miili yote itakua imechukuliwa na ndugu na kuifikisha mahali inapotakiwa kufika, kwa sababu karibia miili yote imeshatambuliwa na familia zao” ameongeza Waziri Mkuu.
Aidha Waziri Mkuu amesema kufuatia kutokea kwa maafa hayo wapo Watanzania kutoka sehemu mbalimbali wameendelea kuahidi kutoa misaada yao kwakua hilo ni tukio la Kitaifa na huku wengine wakitaka kujua namna nzuri ya kufikisha misaada yao.
Aidha kufuatia hilo Waziri Mkuu ametoa angalizo kwamba utoajia wa misaada kwa Wanzatania walioko tayari kuiunga mkono Serikali wahakikishe wanaitumia sasa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa ndio mratibu wa kupokea misaada yote, huku wenyeji watakaotaka kutoa misaada hiyo wataelekeza kwa Mkuu wa wilaya hiyo ambapo ameshaelekeza sehemu ya kupeleka ni kambini pale shuleni walipo waanga.
“Wakuu wa mikoa ya jirani pale ambapo kuna wananchi wamejitokeza kutoa misaada, wakuu wa mikoa sasa huko wataelekeza misaada mikubwa Kwa kuwasiliana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama pamoja na Katibu Mkuu na timu ya maafa yote iko hapa wawasiliane naye wapewe utaratibu kufikisha misaada hiyo” amesema Waziri Mkuu.
” Nataka tuelewane vizuri, kusitokee makundi yakabeba dhanama hii wakaitumia nafasi hii ya madhara haya wao kwao ikawa fulsa, tunatamani kila mchango wa Mtanzania unafikishwa kwa ajili ya kuhudumia wenzetu waliopata madhara haya iwafikie kama ilivyo na hatutasita kwa yeyote ambaye atatumiavibaya michango hii Kwa kuchukuliwa hatua kali, kwa hiyo niwape matumaini kwamba misaada yote mtakayoitoa au kuletaitarayibiwa vizuri na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hata hivyo amefafanua kuwa Jenista Mhangama atakua Mratibu Mkuu, na Katibu Mkuu wake, na kitengo cha maafa ili kuipokea na kuileta hapa kuiratibu na kuifikisha Kwa waanga.