Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Pwani
KITENGO cha damu salama Tumbi, hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, inatumia chupa 15 kwa siku sawa na chupa 450 za damu kwa mwezi ,hivyo uhitaji wa lita 200 ili kukidhi mahitaji.
Kuelekea siku ya Uhuru Desemba 9 wadau ,kambi za jeshi ,jamii inaombwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wajawazito, watoto chini ya miaka mitano ,majeruhi wa ajali wenye uhitaji wa huduma hiyo katika hospital hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha damu Salama Tumbi Tatu Gemela, ameeleza uhitaji ni mkubwa kwani hospital inapitiwa na barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro ,ajali zinapotokea majeruhi uhitaji huduma ya damu kuokoa maisha yao, pia wodi ya uzazi kwa ajili ya wajawazito wenye uhitaji.
“Nawaomba wananchi na Taasisi za Mkoa huo kujitokeza kuchangia damu siku ya 9 Desemba, zoezi hilo litafanywa kwenye eneo la hospital” amesisitiza Gemela.
Changia damu okoa maisha ya mtoto, mama mjazito na wagonjwa wenye uhitaji.