Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime
Kamanda wa Jeshi la Polisi Tarime/Rorya ACP Mack Njera amewata waamdishi wa habari wasiwe wanyonge katika kutekeleza majukumu yao
Amesema hayo kwenye mdahalo baina ya waandishi wa habari na Jeshi la Polisi juu ya ulinzi na ulinzi na usalama uliofanyika leo katika ukumbi wa Blue Sky Tarime.
Mdahalo huo umeandaliwa na UTPC Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tarime chini ya udhamini wa shirika la IMS.
Kamanda amesema ukarasa ufunuka Kwa kuanzia sasa kwa kuimarisha ushirikiano baina yao na waandishi katika utendaji wa majukumu kazi Kwa kuwa kazi zao zinaendana.
Aidha amesema Kila mmoja anapotekeleza majukumu yake azingatie kanuni na Sheria na kwamba Jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa chache kutokana utunzaji wa ushahidi.
Katika hatua nyingine Kamanda Njela amebaini baadhi ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari katika utekekezaji wa majukumu yao kuwa ni usalama ambapo ametaka uanze Kwa mwaandishi mwenyewe,wamiliki wawape mafunzo ya usalama na kuwapa mavazi maalum.
Ameshukuru UTPC Kwa kuandaa mdahalo huo baina ya Jeshi la polisi na waandishi wa habari ambapo utakuwa na matarajio ya wazo la pamoja Ili kuondoa changamoto na daraja kuu katika kulinda mali za wananchi.