Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Taasisi ya German Society for Tropical Paediatric and International Child Health (GTP) imeendesha mafunzo maalumu ya matumizi ya mashine ya Ultrasound maalumu kwa wataalamu wanaohudumia watoto.
Mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa awamu ya pili ni utekelezaji wa mradi unaolenga kuokoa maisha ya watoto kwa kwa kuzuia vifo vinavyoweza kuzuilika, unaotekelezwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Elsa Kroner-Frescenius Stifftung (EKFS) Katika nchi ya Tanzania, Malawi na Nepal.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa ni ya manufaa sana kwa kuwa asilimia 15 ya wagonjwa wanaotibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ni watoto.
Pia amewaasa washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwa makini ili wapate maarifa na wao wakafundishe waataamu wengine na hatimaye lengo la kupunguza vifo vya watoto liwe limefikiwa.
Awali akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa Idara ya Watoto MNH, Dkt. Monica Appolo alisema mafunzo hayo yanajumuisha washiriki 26 ikiwemo washiriki watatu kutoka Ujerumani na Netherlands pamoja na na wakufunzi saba ambapo wakufunzi watatu wanatoka Ujerumani na wanne ni kutoka MNH