Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na MichezoDkt. Damas Ndumbaro ameshuhudia mchezo kati ya TP Mazembe ya DRC Congo dhidi ya Esperance Sportive de Tunis ya nchini Tunisia ikiwa ni mchezo wa mashindano ya African Football League ambao umemalizika kwa TP Mazembe kuibuka na ushindi wa 1-0.
Mchezo huo umeshuhudiwa pia na Naibu Waziri wa wizara hiyo Hamis Mwinjuma na Katibu Mkuu Bw. Gerson Msigwa Oktoba 22, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Viongozi wengine walioshuhudia mtanange huo ni wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Vilabu na Mashabiki ambao wamejitikoza kwa wingi ukiwa ni mchezo wa pili wa mashindano hayo katika Uwanja huo ambayo yalifunguliwa Oktoba 20, 2023 kwa mchezo kati ya Simba na Al Alhy ya nchini Misri.
– Advertisement –