Nianze kwa kuwasalimu wasomaji wetu ambao mmekuwa mkifuatilia safu hii kwa umakini mkubwa. Niwashukuru kipekee wote wanaonipigia simu, kuniandikia ujumbe mfupi (SMS) na baruapepe. Michango yenu wasomaji ina msaada mkubwa sana katika maeneo matatu.

Mosi, inanipa taarifa kwamba ninachokiandika kinasomwa.

Pili, wasomaji wanaponipongeza, kunikosoa ama kujadili nami kuhusu chambuzi zangu mbalimbali inanipa kujitathmini, kujifunza, kujirekebisha na kujinoa zaidi. Tatu, mirejesho hii imekuwa moja ya machimbuko makubwa ya makala nyingi ninazoandika hapa.


Yaani kuna wakati ninapojadili jambo na msomaji napata mada ya kuiandika na wapo wasomaji ambao pia huniomba na kunishauri kuandika jambo hili ama lile. Na ninapoona inafaa na kuna hitaji basi nalichambua. Kwa maana hii nawasihi msichoke kuwasiliana nami wakati wowote tushirikishane nami nijifunze kutoka kwenu, kwani ninayajua machache mno ikilinganisha na mengi mliyonayo ninyi kwa ujumla wenu.


Makala hii leo ninaileta ikiwa ni maombi ya muda mrefu kutoka kwa wasomaji mbalimbali nchi nzima. Ndugu Prasdus Muyinga kutoka Mafinga aliniandikia mwezi Juni, “Bwana Sanga, Mungu akubariki sana kwa kazi kubwa unayoifanya. Hakuna mtu wala kampuni inayoweza kulipa kikamilifu thamani ya maarifa unayotupatia. Ninaomba ukipata wasaa utuchambulie hiki kitu kiitwacho biashara ya mtandao.”


Msomaji mwingine kutoka Dar es Salaam aliniandikia baruapepe ndefu kweli akieleza kuwa yeye ni mmoja ya watu wanaofanya biashara ya mtandao. Msomaji huyu kwa maelezo yake aliniambia kuwa anadhani Watanzania wengi bado hawajaijua fursa hii ambayo inampa mtu wasaa wa kuzalisha fedha nyingi kwa kutumia muda na nguvu kidogo.


Msomaji aliyenifanya niinue kalamu na kuandika makala hii ni mwenye namba 0717 366 590 ambaye aliniandikia hivi: “Nina uhakika Watanzania na viongozi wa serikali yetu wanatambua mchango wako mkubwa wa kuzikomboa fikra za Watanzania ili zijitegemee. Lakini kabla ya mwaka huu haujaisha nitakuwa mmoja ya wasomaji watakaofurahi sana ikiwa nitasoma uchambuzi wako kuhusu biashara ya mtandao (network marketing).”


Kwanza kabisa ni kuwa biashara hii ya mtandao (Network Marketing) ninaifahamu vizuri kwa maana ya kuhudhuria semina zake na kufanya kwa vitendo. Hata hivyo, sikuwa nimebaini kuwa ni fursa ambayo inaweza kuhitajika na watu wengi. Leo ngoja tushirikishane mambo mawili-matatu kuhusu biashara hii.


Tukitazama mzunguko wa fedha duniani unahusishwa na makundi makubwa manne ya shughuli tuzifanyazo kila siku. Kundi la kwanza ni kundi la waajiriwa ambalo linahusisha watu wengi kuliko kundi lolote kutokana na mapokeo na mfumo wa elimu uliopo. Ajira ikiwa ni mojawapo ya fursa yakutengeneza kipato bado inachangamoto nyingi ambazo zinamfanya mtu ashindwe kuishi ndoto zake na malengo aliojiwekea.


Uzoefu na utafiti vinabainisha wazi kuwa kipato cha ajira pekee yake hakiwezi kutimiza ndoto kubwa tulizonazo katika maisha na ndio maana kila kukicha mawazo ya binadamu yapo katika kutafuta fursa nyingine za kujipatia kipato cha ziada. Kundi la pili ni la waliojiajiri wenyewe. Mtazamo mkubwa wa mtu kujiajiri mwenyewe ni imani kwamba ukitaka jambo lifanyike vizuri lifanye mwenyewe.


Changamoto kubwa ambayo anakutana nayo mtu aliejiajiri ni kutokuwa na kipato endelevu, kwa maana ya kwamba shughuli nyingi za kujiajiri zinahitaji uwepo wako kwenye biashara yako muda wote na pengine usipokuwepo unaweza kukosa kipato. Kundi la tatu ni kundi la wamiliki wa biashara kubwa.


Hawa ni watu ambao wamewekeza kwenye rasilimali watu na siri kubwa ya mafanikio yao ni wanamiliki mtandao mkubwa wa watu ambao ufanyaji kazi wa watu hao ndio nguvu kazi ya ukuaji wa biashara zao. Kundi la nne ni la wawekezaji. Kundi hili ni la watu ambao wameshafikia kwenye uhuru wa kipato kwa kuwa wamewekeza kwenye vitu vinavyopanda thamani.


Kwa mtazamo halisi ni kwamba makundi mawili ya mwisho kundi la wamiliki wa biashara na kundi la wawekezaji ndio makundi ambayo watu wengi wana mtazamo wa kufikia malengo kwa hayo. Changamoto kubwa ni fursa gani mtu anaweza kuitumia kufika hapo.


Biashara ya mtandao ni mfumo wa biashara ya usambazaji wa bidhaa au huduma kwa njia ya upashanaji habari. Kwa kuwashirikisha watu kuhusu ubora wa bidhaa au huduma, na kuhusu fursa ya biashara ya mtandao na wakaamua kununua bidhaa au huduma au wakaamua kuwa wafanyabiashara ya mtandao unatengeneza kipato.


Biashara hii ya mtandao ni fursa mpya duniani na inashauriwa (most recommended) na wataalamu na wafanyabiashara wakubwa na wadogo duniani kote. Namna biashara hii ilivyo ni kuwa inatoa nafasi ya mtu kutengeneza mfumo wa biashara kwa kusambaza bidhaa na huduma miongoni mwa watumiaji moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji.


Wakati nilipoisikia biashara hii nilipata hamasa ya kujiunga nayo. Licha ya kuwa nimefanya biashara hii kwa miaka kadhaa katika kampuni tofauti; wakati nikijiandaa kuandika makala hii nilimtafuta mmoja ya vijana waliofanikiwa sana katika biashara hii. Kijana huyu ni rafiki yangu, anaitwa Amedeus Deus, anafanya biashara hii na Kampuni ya Forever Living.


Kwa wote watakaopenda kuchangamkia fursa hii nitawakutanisha moja kwa moja na kijana huyu mwenye masikani yake mjini Iringa. Uzuri wa biashara hii ni kuwa anayekuingiza biasharani anaweza kukusaidia na kufanya naye biashara ya mtandao akiwa mahali popote na wewe ukiwa mahali popote. Ndio maana inaitwa biashara ya mtandao.


Zipo kampuni kadhaa hapa Tanzania ambazo zimeingia kutoka Ulaya na Marekani zikifanya biashara ya mtandao. Nimeamua kuichambua biashara ya bidhaa za Forever kwa sababu nimeukubali mfumo wake wa kibiashara, namna wanavyotoa ‘commission’ pamoja na umakini wao.


Kampuni ya Forever Living Products ambayo makao yake makuu yapo nchini Marekani ilianzishwa mwaka 1978 na sasa inafanya biashara ya mtandao katika nchi zaidi ya 150 duniani. Hapa Tanzania kampuni hiyo ilianza rasmi mwaka 2007.


Kampuni hii inaongoza duniani kwa kuzalisha bidhaa za asili zitokanazo na mmea wa Aloe Vera na asali itokanayo na nyuki wadogo. Kutokana na wingi wa bidhaa wanazozalisha wametenga bidhaa zao kwenye makundi tofauti; bidhaa za vinywaji, virutubisho, usafi na utunzaji wa ngozi, bidhaa za kudhibiti uzito na za urembo.


Utofauti iliopo kwenye bidhaa zao ni ubora endelevu wa hali ya juu uliothibitshwa na mihuri mbalimbali katika nchi 150. Mojawapo ya swali la mwanzilishi na mmiliki wa kampuni, Rex Maughan, lilikuwa mojawapo ya sababu ya ongezeko la watu kuwa na maradhi duniani ni kutokana na kukosa kipato mfukoni.


Msukumo wa changamoto hiyo ulichangia kuanzishwa kwa kampuni ya Forever kwa nia ya kuwapatia watu fursa itakayowapatia afya bora na kipato halali. Kupitia mfumo wa biashara ya mtandao kampuni hiyo inampatia mfanyabiashara fursa ya kutengeneza vipato vingi tofauti.


Kuna faida mbalimbali mtu unazoweza kupata kupitia biashara hii ikiwamo faida ya mauzo ya bidhaa rejareja ya asilimia 43%, bonasi inayotokana na ununuzi utakaofanywa na wewe mwenyewe na mtandao wako, yaani bonasi ya timu. Kupitia kipato hiki mtu anaweza kutengeneza kipato cha zaidi ya Sh milioni tatu kwa mwezi.


Kwa ngazi ya kwanza, mtu anapoanza biashara atatambulika kama msimamizi  msaidizi (assistant supervisor) ambapo anaweza kutengeneza kipato cha mpaka Sh 300,000 ikifuatiwa na ngazi ya msimamizi mkuu ambapo mtu anaweza kutungeneza kipato cha mpaka Sh 700,000.


Ngazi nyingine inayofuata ni Meneja Msaidizi, ambapo katika ngazi hii mtu ana uwezo wa kutengeneza kipato cha mpaka Sh milioni 1.5 ikifuatiwa na ngazi ya juu ya Meneja, ambapo mtu ana uwezo wa kutengeneza kipato cha zaidi ya Sh milioni mbili.  Vipato vyote vya bonasi ya timu unavitengeneza kila mwezi.


Pia kuna faida ya asilimia 21.5 itokanayo na msambazaji mpya ambayo ni jumla ya Sh 120,000 kwa kila mtu mmoja ambaye atakuwa ameamua  kufanya biashara. Pamoja na hiyo, ipo bonasi ya gari ambayo unafikisha vigezo vya kuipata ikiwani  utatengeneza kipato cha kuanzia Sh 600,000 mpaka Sh 1,200,000 kwa miezi 36. Kama nilivyoeleza vyeo vinavyofikiwa (hapo juu) fursa hii ya kupatiwa gari ni ikiwa utafikia cheo cha umeneja.


Vilevile kuna bonasi ya uongozi ambayo ni aina nyingine ya kipato ambacho mtu anaweza kutengeneza kwa namna anavyoweza kutengeneza viongozi wengine ndani ya timu yake. Kipato kingine ni gawio la faida ambalo hutokana na asilimia 100 ambazo kampuni itatengeneza mwisho wa mwaka, asilimia 60 huwa zinarudi kwa wafanyabiashara wote walioweza kufanya biashara kubwa zaidi.


Pia kampuni hii inatoa nafasi ya matukio ya kutambuliwa na safari za kimataifa za mapumziko hutolewa na kampuni kila mwaka kwa wafanyabiashara wa kampuni  walioweza kukuza biashara zao vizuri.


Ushiriki wa mfanyabiashara kwenye safari hizo za mapumziko unagharimiwa na kampuni kwa maana ya nauli ya kwenda na kurudi, malazi na fedha ya mfukoni ya kujikimu. Kwa ujumla wa vipato vyote na utofauti wake vinatokana na ununuzi wa bidhaa ambayo mfanyabiashara ataufanya pamoja na mtandao wake (timu yake).


Upekee wa mfumo huu wa biashara ni kwa sababu kwanza, mtu anaweza kutumia mtaji mdogo sana kuanza biashara. Pili, mtu anaweza kuanza biashara kwa muda wake wa ziada bila kuacha shughuli anayofanya. Tatu mtu atapewa msaada kutoka kwa waliokutangulia na semina za mafunzo kutoka kwenye kampuni kuhusu bidhaa za kampuni, mbinu na utaratibu wa kuijenga biashara yako.


Mwisho, niwahamasishe Watanzania wote kuchangamkia fursa hii pamoja na nyingine kila mara mnapopata taarifa ama wasaa.

“mailto:[email protected][email protected] 0719 127 901