“Siku hizi kuna watu wengi mno ambao huingia katika chama na kugombea nafasi za uongozi kwa matumaini ya kupata fedha na vyeo kwa faida zao wenyewe. Moyo wa kujitolea umefifia mno. Katika hali kama hiyo ni vigumu sana kuwapata viongozi wenye moyo wa kuwatumikia wenzao.”
Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akikemea tabia ya wanaotafuta uongozi kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Alizaliwa Aprili 13, 1922 kijijini Butiama, Mara, alifariki Oktoba 14, 1999 jijini London, Uingereza.
Princess Diana: Kuvumiliana kumetoweka
“Tatizo kubwa katika Dunia ya leo ni kutovumiliana. Kila mmoja siyo mvumilivu kabisa kwa mwingine yeyote.”
Hii ni kauli ya Princess Diana, maarufu kama Mfalme wa Wales, alipoeleza kutofurahishwa na kufifia kwa dhana ya kuvumiliana katika jamii. Alizaliwa Julai 1, 1961 huko Sandringham, alifariki Agosti 31, 1997, Paris, Ufaransa.
George Bush: Serikali haileti utajiri
“Serikali haiwezeshi utajiri. Jukumu kubwa la serikali ni kuweka mazingira yanayowezesha watu kupanua kiwango cha kazi…”
Rais wa 43 wa Marekani, George Walker Bush, aliyasema haya kuwakumbusha watu kutambua jukumu la serikali siyo kuwaletea utajiri. Alizaliwa Julai 6, 1946 huko New Haven.
Lucille Ball: Bora kujua usiyoyaweza
“Nadhani kujua usiyoweza kuyafanya ni muhimu zaidi kuliko kujua unayoweza kuyafanya.”
Maneno haya ni ya msanii mwigizaji maarufu wa nchini Marekani, Lucille Ball. Alizaliwa Agosti 6, 1911 huko Jamestown, alifariki Aprili 26, 1989 Los Angeles, California.