Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma
ZAIDI ya watu 20,000 wameripotiwa kung’atwa na mbwa kwa kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu ambapo mkoa wa Dar es Salaam unaongoza ukifuatiwa na mikoa ya Dodoma , Morogoro na Arusha.
Jumla ya dozi 180,000 za chanjo ya kichaa cha mbwa zimesambazwa katika halmashauri 26 nchini kuanzia septemba mwaka huu ambapo jumla yam bwa 20,426 na paka 740 wamekwishakuchanjwa.
Hayo yameelezwa leo Sept 28,2023 wakati wa siku ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa duniani iliyofanyika katika wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Arbogast Warioba alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti 201,2023 jumla ya watu 20,005 walitolewa taarifa ya kung’atwa na Wanyama.
Amefafanua kuwa mikoa hiyo inayoongoza kuwa na matukio ya kung’atwa na Mbwa ni Dar es Salaam, matukio 3,321, Dodoma matukio 3,136,Morogoro matukio 1,559, na Arusha matukio 1,155 na takwimu hizo zinajumuisha wananchi waliopata huduma katika vituo vya afya.
Pia amesema ugonjwa wa kichaa cha mbwa unakadiriwa kusababisha takribani vifo 59,000 kwa mwaka duniani, ambapo asilimia 36 ya vifo hivyo hutokea katika bara la Afrika, pia asilimia 30 hadi 50 ya waathirika wa ugonjwa huo ni watoto chini ya miaka 15 kwasababu ndio huwa karibu na mbwa wanaofugwa kwa muda mwingi, pia hupenda kucheza,kuchokoza mbwa wasiomfahamu njiani.
“Vimelea vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa vinapoingia katika jeraha hushambulia mfumo wa fahamu kuanzia katika eneo la jeraha, kuelekea katika uti wa mgongo na hatimaye kuathiri mfumowa kati ya fahamu (ubongo)” amesema
Amesema kuwa katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo serikli imeendelea kutoa elimu kwa umma, kuboresha utekelezaji way a afya moja nchini, kurahisisha upatikanaji wa huduma za chanjo ya kichaa cha mbwa kwa wananchi.
Pia kurahisisha upatikanaji wa huduma ya chanjo kwa Wanyama hasa mbwa nap aka.
Pia alisema kuwa serikali imeshiriki katika michakato ya kidunia ambayo imewezesha mwaka huu 2023 Shirika la Usambazaji Chanjo Duniani (GAVI) kuridhia chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha mbwa (Anti -rabies) kuingizwa katika mfumo wa chanjo za kawaida ambapo gharama zinatarajiwa kushuka zaidi pale taratibu za utekelezaji wa jambo hilo utakapokamilika.
Kawa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya mifugo ngazi ya jamii Stanford ameeleza kuwa ameeleza ugonjwa huo huishi kwenye baadhi ya Wanyama wa porini ikiwemo popo ambapo husambaa kupitia Wanyama wa nyumbani kwa kuambukizwa.
“Mbwa na Wanyama wengine wenye virusi vinavyosababisha kichaa cha mbwa huweza kuambukiza bila kuonesha dalilizozote,hivyo ni muhimu mtu yeyote aking’atwa na mbwa au mnyama mwingine atoe taarifa kwa mtaalamu wa mifugo ili hatua husika zichukuliwe,”amesema
Naye, mwakilishi wa wizara ya Afya Dk.Robert Kishimba amesema mbali na juhudi za kuutokomeza ugonjwa huo bado ni janga na hivyo ni lazima kuuepuka kwa kuwakinga Wanyama kama mbwa,paka na wengine .
Aidha jamii inapaswa kuepuka tabia hatarishi za kumchokoza mbwa au kumpiga ikiwa ni pamoja na kuelimisha watoto wwasicheze na mbwa wasiyemfahamu.
Naye mtaalamu wa magonjwa ya mbwa Ofisa mifugo wilaya ya Kongwa Dk.Kisimba Benjamin ameeleza kuwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa huanza kipindi cha baridi ambapo dalili zake ni mbwa kutoa ute usioisha,mbwa kung’ata vitu ovyo,kuogopa maji,kubadili tabia na kupoteza fahamu .