Na Mwandishi Wetu, JamhutiMedia, Geita
Kampuni ya Franone Mining and Gems Ltd inayojihusisha na uchimbaji wa kati wa madini ya Tanzanite na Spinel kwenye Sekta ya Madini imekaribisha wadau kujionea upekee wa madini hayo na hasa madini ya Tanzanite yanayochimbwa Tanzania.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Meneja mgodi wa Kampuni ya Franone, Vitus Ndakize, leo Septemba 26, 2023 kwenye Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini katika Viwanja vya Bombambili Geita, amesema kuwa kampuni hiyo iliyoanza tangu mwaka 2011 imekuwa na rekodi ya kutoka katika uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati.
Akizungumzia na baadhi ya vyombo vya habari kwenye maonesho hayo, Vitus ameshukuru Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa miongozo na maelekezo kwa wachimbaji wadogo kupiga hatua kutoka uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wakubwa.
“Kutokana na jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan alizozifanya kwenye Sekta ya Madini tumeweza kuinuka wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati.
Akieleza mipango ya Kampuni amesema kuwa wamejiwekea kukua zaidi na kutengeneza ajira nyingi kwa Watanzania pamoja na kuendelea kuongeza migodi katika mikoa mingine.
Vitus amesema kuwa wana Ofisi katika mkoa wa Manyara na Morogoro wanapatikana kwa mawasiliano ya namba za simu 0742206648 na email [email protected].