Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amealikwa kuwa mgeni maalum kwenye mkutano wa 52 Jumuiya ya Waislam Waahamadiyya utakaofanyika tarehe 29 Septemba mpaka Oktoba Mosi, mwaka huu katika .kijiji cha Kitonga Msongola jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 28, 2023 jijini Dar es Salaam, Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahamadiyya Tanzania, Shekh Tahir Mahammod chaudhiry amesema katika kuazimisha siku hiyo amewataka Waislam Hamadiyya kuweka mafungamano madhubuti na khilafat watoe shukrani endelevu kwa mwenyezi Mungu.
Amesema hawapaswi tu kusali sala za dhati na shukrani kwa Mungu ,bali wanapaswa kuweka kiapo kizito kwamba watajishughulisha na matendo mema ya kheri na kujitahidi kuwa Waislam wa Ahamadiyya wa kutolewa mfano.
“Kumbukeni mafanikio yenu yanatokana na kushikilia kamba ya mwenyezi Mungu na kushikamana na taasisi ya ukhalifat _Ahamadiyya ,ambapo inawakilisha ukhalifa pekee wa kweli na wa haki Kwa Waislam kufuata uaminifu mwongozo wa khalifat-ulmasih ndipo tutaweza kuufahamisha ulimwengu kuhusu mafundisho safi na ya kweli ya uislam”amesema.
Amesema lwa sasa wanapaswa kuangalia chanel ya MTA mara kwa mara na kuzihimiza familia zao,hasa watoto itawawezesha kudumisha uhusiano wa kudumu na kuimarisha imani za dini yao.
Ameongeza kuwa wanapaswa kuzingatia wajibu wao kuhusu mahubiri ambayo ni muhimu kwa kila Ahamadiyyya na kupanga busara na kubuni njia mpya za hekima za kueneza ujumbe wa amani kote nchini na nchi jiani.
“Mwenyezi Mungu akuwezesheni kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha yenu kwa kuelekea ucha- Mungu,ikiwemo tabia njema, matendo mema na ubinadamu, ” amesema.
Amir Mkuu wa Ghana Mohamamed Bin Salih Ahamadiyyya amesema mkutano huo utasadia kujenga umoja na mshikamano wa kindugu miongoni mwa waislam Ahamadiyya duniani kote.
Amesema washiriki watawapa nafasi ya kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kiimani na kibiashara.
Naibu Amir Abdulrahman Ame akisoma hotuba kwa niaba ya Amir na Mbaashiri Mkuu Shekh Tahir Chaudhiry ,amesema mkutano huo unalengo la kukuza udugu maelewano mema na ufahamu wa pamoja kama matarajio ya Jalsa Salana mwanzilishi wa Jumuiya ya Waislam Wahamadiyya Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad Ame amesema mkutano pia utasadia kuongeza hofu ya mwenyezi Mungu miongoni mwa washiriki Ili kuepukana na mabaya kupata moyo wa huruma na kuongeza upendo, unyenyekevu ukarimu baina yao Ili tabia ya kweli ipatikane ndani yao
“Kupitia mkutano huu waumini watapata nafasi ya kusikiliza hotuba na nasaha za wataalam wa jumuiya ,ambapo miongoni mwa mada zitakazotolewa ni namna bora ya kuwalea watoto ikiwemo kujali elimu ya dini na kujitahidi kuwa raia wema Ili kuishi kwa amani na kuwa watiifu kwa sheria za nchi “amesema.
Amesema mada nyingine ni juu ya kuwasihi waumini kutochanganya dini na siasa kwani jambo hilo ,huleta mkanganyiko na kuzalisha mianya kwa wanasiasa kuitumia dini vibaya kwa maslahi yao binafsi.
Amesema mkutano huo utafanyika siku tatu nakufikia kielel tarehe mosi oktoba katika Kijiji cha kitonga Msongola ‘ na unatarajiwa kuhudhuliwa na washiriki 5000 mpaka 6000 kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo kauli mbinu ya mkutano wa mwaka huo ni ‘Tawheed ya kweli haiwezi kusimamishwa bila ukhalif’