Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo yavMakazi Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani Bw. Patrick Kipalu.
Dkt Mabula amekutana na mkurugenzi huyo anayeshughulika na Programu za Haki na jitihada za Rasilimali Ardhi katika Bara la Afrika katika ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 29 Agosti 2023.
Mazungumzo ya viongozi hao mbali na mambo mengine yamelenga maandalizi ya Kongamano la Nne la Kimataifa litakalofanyika jijini Arusha kuanzia 12- 15 Sept 2023 likiwa na agenda kuu ya upatikanaji wa hatimilki za ardhi.
Taasisi hiyo ya Marekani ndiyo wadhamaini wa kongamano hilo linalojadili masuala mbalimbali yahusuyo masuala ya ardhi ikiwemo hati milki za ardhi.