Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es Salaam
Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha afya kimesema jeshi hilo linatoa huduma za kiafya kwa wananchi na askari pamoja na familia za askari wa maeneo tofauti tofauti licha ya kazi yake ya msingi ya kuwalinda raia na mali zao hapa nchini.
Hayo yamesemwa na afisa mnadhimu namba moja wa kikosi cha afya Kamishna Msadizi wa Polisi ACP daktari Salum Luyeko ambaye ni daktari bingwa magonjwa ya kike kuwa askari hao wameonyesha moyo wapekee kwa Hosptali hiyo na amewaomba kuendelea na moyo huo wa kutoa misaada kwa jamii.
Dakatari Luyeko ametoa rai kwa makundi mengine kufika katika hospatali hiyo ambayo inatoa huduma kwa makundi yote ambayo yanafika katika hosptali hiyo huku akibainisha kuwa askari hao wameonyesha njia ya kwa askari wengine kutembelea hospatali kuu ya Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Isack Mulilo ambaye ni mkufunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) amesema kuwa wao waliona vyema kuungana kama askari walioajiliwa Pamoja kuungana na kutoa mchango wao na kufariji wagonjwa hosptali kuu ya Jeshi la Polisi.
Nae mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Aisha Wisley amesema kuwa wamekuwa na utaratibu huo kila mara kutoa msaada kwa makundi tofauti tofauti ndani ya Jamii ambapo kwa kipindi hiki waliona watoe msaada na kuwafariji wagonjwa katika Hosptali Kuu ya Jeshi la Polisi iliyopo Kilwa Road jijini Dar es Salaam.