j

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa na Afrika Mashariki alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma tarehe 19 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023.
Viongozi na Watendaji wa Taasisi mbalimbali wakisikiliza na kufuatilia kwa makini Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023