Shirika la nyumba la Taifa (NHC) limeingia makubaliano na waratibu wa taarifa sahihi za waombaji wa mikopo ‘CREDIT INFO BUREAU’ ili kupeleka majina ya wadaiwa sugu wasiweze tena kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha ikiwemo mabenki.

Hayo yamesemwa leo Agosti 15, 2023 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya

Amesema Shirika hilo,  linadai jumla ya sh bilioni 23 kutoka kwa taasisi za serikali na watu binafsi ambapo kuna wapangaji sugu 3,000 ambao wameshawasilsiha taarifa zao kwenye ‘Credif Info Bureau’ kwa hatua za awali na wamewapa notisi ya mwezi mmoja kulipa madeni yao kabla hawajawatangaza hadharani.

Pia, katika kukusanya madeni hayo NHC imetangaza kampeni ya mwezi mmoja kuanzia leo itakayoongozwa na kauli mbiu ‘Lipa Madeni yako kwa Maendeleo ya  Shirika na Taifa Letu’

Amesema  awali madeni yalikuwa  Sh bilioni 28 na mbinu mbalimbali yalizotumia kukusanya madeni hayo  zimesaidia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 5 kutoka kwa wadaiwa na sasa kubakiwa na deni la sh bilioni 23.

Nae, Mkurugenzi wa Usimamizi na Umiliki wa NHC, Elias Msese akifafanua madeni hayo amesema  katika deni la sh bilioni 23 Taasisi za serikali zinadaiwa sh bilioni 3 na sh bilioni 18  zipo katika madeni ambayo wateja wake 3,000 wamekimbia si wapangaji tena wa NHC  na zilizosalia zipo kwa wateja ambao bado ni wapangaji wa NHC na tayari wameingia nao makubaliano ya kulipa malimbikizo ya madeni yao.

“Taasisi za serikali zinadaiwa sh bilioni 3, hizi ni zile ambazo zilihamishwa kwenda Dodoma, serikali sio mdaiwa sugu, madeni yaliyobaki ni ya watu mbali mbali ya wapangaji wetu, wamekimbia na kuacha madeni kwenye nyumba zetu ndio hawa tunaowatafuta kwa kutumia taarifa zao kutoka Brela, Nida na taarifa walizojaza kwenye fomu zetu wakati wanaomba upangaji.”Amesema na kuongeza

“Madeni ya serikali ni asilimia 14 tu ya kiasi chote cha fedha tunachodai na tayari yameshahakikiwa madeni yote yatalipwa mwaka huu wa fedha, imeundwa kamati ya wakurugenzi wanne ambao wamepewa jukumu la kufuatilia ili fedha hizo zilipwe,” amesema na kuongeza Wateja 3,000 wakacha deni la bilioni 18 NHC, wasakwa

“Katika deni la sh bilioni 23, waliokimbia wanachukua deni la takribani sh bilioni 18 waliopo ndani hali sio mbaya, tumeingia nao mikataba wanalipa kodi ya mwezi na wanapunguza madeni yao.” Amesisitiza

Aidha, Msese amesema, kwa sasa wameanzisha mfumo wa kuwafutiali wateja wasumbufu kupitia mifumo yao na kwamba mkataba wake utakapoisha hawatampa mkataba mpya.

“Mikataba yetu kwa sasa ni miaka mitatu mitatu, ikiisha kabla hatujamuongezea tunamuangalia ulipaji wake kodi kama ni msumbufu hatumpi mkataba mpya, lakini pia kwa wapangaji wapya kwa sheria zetu za sasa wanalazimika kulipa amana ya nyumba anayoipangisha kwa kulipa kodi ya miezi mitatu ndio tumpe mkataba.”Amesema Msese

Akizungumzia Kampeni hiyo ya kukusanya mapato na Meneja wa Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya amesema Shirika limeamua  kuanza kampeni ya kukusanya madeni hayo kwa kuingia mikataba na Wapangaji ya kuwaruhusu kulipa madeni yao kwa awamu. kila mpangaji anayodaiwa na kama ana sababu maalum ahakikishe anaweka utaratibu madhubuti wa kulipa madeni yake anayoidaiwa.

Pia,  kwa wapangaji waliopo kwenye nyumba ambao watashindwa kulipa  kodi na malimbikizo yao ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa, atakuwa ameonyesha kuwa haihitaji nyumba anayopanga na Shirika litavunja mikataba yao ya upangaji na kuwaondoa kwenye nyumba kwa mujibu wa sheria.

Aidha, kwa wapangaji ambao walishapewa notisi mbalimbali za kulipa kodi wanayodaiwa, utekelezaji wa notisi hizo unaendelea kama notisi hizo zinavyoelekeza.

“Hivyo, Shirika linawasihi watekeleze wajibu wao ili kuepuka usumbufu utakaoweza kujitokeza kwa kushindwa kutimiza wajibu huo.

Pia kuanzia sasa Mpangaji yeyote mpya hawezi kupangishwa bila kulipa amana ya pango (security deposit) ya miezi mitatu.

Amesema, kwa wapangaji waliopo kwenye nyumba na ambao hawajakamilisha kulipa amana ya pango inayotakiwa wameandikiwa barua na kupewa muda mpaka Desemba 31, 2023 ili wakamilishe kulipa amana za pango vinginevyo Shirika litalazimika kusitisha mikataba yao ya upangaji.

Saguya amesema, ili kuepusha madeni ya mara kwa mara, kuanzia sasa Shirika halitampa mkataba mpya mpangaji ambaye anakuwa na rekodi mbaya ya kulipa kodi kwa wakati. Watanzania wengi wamekuwa wakiomba upangaji katika nyumba kuwa wapangaji wa NHC.

“Wadaiwa sugu watakaokaidi maelekezo haya ya Shirika, watakuwa wameruhusu Shirika kuwatangaza katika vyombo vya habari ili Mashirika na makampuni mengine yasiingie kwenye makubaliano ya kibiashara na mtu au kampuni inayodaiwa.

“Ili kuhakikisha kodi na malimbikizo ya madeni yanalipwa, Mkurugenzi Mkuu ameunda Kamati ya Menejimenti ambayo itaanza kazi rasmi wiki hii ya kufuatilia madeni yote yanayodaiwa na Shirika.” Amese