Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma
Kutokana na ukamilishwaji wa miradi ya kimkakati na miradi midogo midogo ya kusogeza huduma kwa wananchi,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeweza kufikia zaidi ya wakazi laki saba ambao hapo awali hawakuwa na huduma
bora za majisafikwa mwaka2022/23.
Hayo yameelezwa leo Agost11,2023 Jijini Dodoma na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Kiula Kingu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi na kueleza kuwa ndani ya mwaka wa fedha 2022/23 DAWASA imetekeleza jumla ya miradi 10 ya
kimkakati na zaidi ya miradi midogo midogo 86 ya kusogeza huduma kwa wananchi.
Alisema miradi hiyo ilihusisha kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa, kujenga matenki makuu
yakuhifadhi maji, kujenga vituo vya kusukuma maji nakuongeza mtandao wa mabomba ya maji ili maji yanayozalishwa yaaweze kufikia wananchi ndani ya eneo la huduma.
“Miradi mikubwa iliyo tekelezwa na kukamilishwa 2022/23 ni pamoja na,mradi wa ujenzi wa mfumowa usamabzaji maji kati ya Bagamoyo hadimatenki yaliyopo jirani na Chuo kikuu cha Ardhi, mradi wa maji Kigamboni, mradi wa maji Chalinze awamu ya tatu na mradi wa maji Mshikamano,;
Mwingine ni mradi wa maji nje ya mtandao(unaohudumia mitaa 12), mradi wa maji Mbezi Makabe,mradi wa maji Zegereni, Mradi wa maji Soga, Mradi wa maji Mbwawa nmiradi ya maji 14 iliyotekelezwa chini ya programu ya lipa kwa matokeo,”alisema.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa miradi hiyo ambayo ina uweo wa kuhudumia wakazi 722,308 katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani ilijengwa kwa gharama ya jumla shilingbilioni219.4.
Kuhusu vipaumbele vya DAWASA kwa mwaka wa fedha 2023/2024, alisema imejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati saba ikiwemo wa bwawa la Kidunda, Mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji.
Alitaja mingine kuwa ni wa maji Kwala, Mradi wa maji Mji wa Pangani Kibaha, Ujenzi wa mradi kutoka
Kimbiji-Kigambonihadi jirani naChuo cha Uhasibu T.I.A, Ujenzi wa mradi wa maji Kusini mwa Jiji la Dar es salaamna Mradi wa uchimbaji visima virefu tisaeneo la Kigamboni.
“Miradi hii itakayotekelezwa kwa jumla ya Tsh.Bilioni 425.9 ina inalenga katika; kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa na DAWASA,kuo6ngeza uwezo wa kuhifadhi maji, kuimarisha mfumo wa usambazaji majina kuimarisha huduma katika maeneo ambayo hayana mtandao hasayale ya pembezoni,”alisema
Kuhusu utekelezaji wa utunzaji wa mazingira alisema DAWASA imekuja na ubunifu wa kujenga mifumo na mitambo midogo midogo ya kuchakata majitaka inayojengwa maeneo ya pembezoni ambapo zaidi yalita 780,000 za majitakazitakuwa zikichakatwa kwa siku.