Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi-Tanga

Jeshi la Polisi limesema litaendelea kushirikisha Jamii katika kupambana na uhalifu katika maeneo mabalimbali hapa Nchini huku likipongeza wadau wenye mapanzi mema na Jeshi hilo kwa mashirikiano wanayoyaonyesha katika Mapambano dhidi ya uhalifu

Hayo yamesemwa leo Agosti 10,2023 Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kamishna Msaidizii Mwandamizi wa Polisi SACP- Dkt.Lazaro Mambosasa wakati alipotembelea viwanja vya mafunzo na mbinu za Medani za kivita eneo la Mkomazi Mkoani Tanga.

SACP Mambosasa amewapongeza islamic help kwa mafano mzuri waliouonyesha wakuchimba kisima katika viwanja hivyo vilivyopo eneo la Mkomazi ambapo amewaomba wananchi kuendelea kuiga mfano mzuri ulionyeshwa na islamic help.

Kwa upande wake balozi wa Maji kutoka Tanga Habibu Mbota amesema wanaendelea na uchimbaji wa kisima hicho ambacho tayari kimeonyesha dira ya upatikanaji wa maji hayo ambapo wamehadi siku chache zijazo watayafikia maji hayo ambayo yatatumiwa na askari wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi ambao ni zaidi ya elfu moja katika kambi hiyo ya mafunzo ya medani za kivita Mkomazi.

Nae Rashid Juma mkazi wa Mkomazi amelishukuru uwepo wa Jeshi la Polisi katika eneo la mkundi mbaro Mkomazi ambapo amesema kwa kuchimbwa kisima hicho kitakuwa msaada mkubwa kwao.