Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar

Taasisi na jumuiya za kiislamu Tanzania, haikubaliani na hatua ya Serikali kusimamia dini ya kiislamu na kuifundisha

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2023, Amiri Jumuiya na Taasisi za Kislamu Tanzania Alhajj Sheikh Musa Kundecha, amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kwamba,Serikali sasa imekwishaandaa silabasi za masomo ya dini na kuondoa mambo yote ya imani ya dini inayohusiana na dini hizo.

Amesema kwamba katika kikao chao cha Julai 23/7/2023 kilichofanyika Masjid EFA viongozi wa jumuiya na taasisi za kislaam walipokea kwa mstuko mkubwa taarifa kwamba Serikali sasa inasimamia dini na kufundisha.

“Mstuko huu unakuja katika ukweli kwamba kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, serikali haina dini na kuwa mambo ya dini yapo nje ya utendaji wa Serikali na kila dini itasimamia mafunzo ya dini yake na kwa kuzingatia kwamba dini na masomo yake yalipangwa kwa pamoja baina ya taasisi za dini na Serikali kupitia vitengo vyake vya elimu na kuandaa silabasi na vitabu vya kufundishia” amesema Sheikh Kundecha.

Sheikh Kundecha amesema kwa mujibu wa historia ya masomo ya dini na kufundishwa kwake,ilikwishatokea Serikali kuingilia masomo ya dini na wasilamu kupinga kuingiliwa huko hatimaye kukubalika masomo ya dini yataandaliwa kwa pamoja baina ya wananchi na Serikali na kupatikana silabasi na vitabu kuanzia ngaizi ya wali hadi vyuo vya ualimu.

”Sasa jambo hili linatulazimisha kuamini kuwa serikali inakuja na mfumo wa dini mpya, ikizingatiwa kwamba dini yetu ya kiislamu na serikali ipo tofauti kubwa za misingi”amesema Shekhe Kundecha.

Ametoa mfano kwenye Serikali kuna pombe zote ni halali, wakati katika uislamu pombe zote ni haramu.

Shekhe Kundecha amesema kutokana na uzito wa jambo hilo,walilazimika kumuandikia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kumuomba kukutana ili kulingalia jambo hilo kwa mustakabali wa taifa letu barua ambayo ilifika ofisini kwake Julai 25,2023 lakini mpaka sasa hawajaitwa wala kujibu barua hiyo.

“Serikali yenyewe haina dini na sasa imeandaa, mafundisho ya dini ya kiislamu na kuondoa mambo yote ya kiimani dini ya uislamu bila imani hakuna dini sasa sisi tunaomba waziri akutane nasi ili kujenga mustakabali mwema wa nchi yetu,” amesema.

Please follow and like us:
Pin Share