Na Cresensia Kapinga, JamhuriMdia,Songea

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Songea mjini Dkt. Damas Ndumaro ameonesha kufurahishwa na jinsi wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanavyoendelea kujitokeza kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya mkoani humo kwa ajili ya kupata msada wa kisheria unaotolewa na wanasheria mbalimbali wakiwemo mahakimu na mawakili na Taasisi zisizo za kiserikali zinazotoa huduma za msaada wa kisheria kwenye kampeni ya Mama Samia Legal Eid inayoendelea.

Waziri Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya majimaji vilivyopo manispaa ya Songea, ambako kampeni hiyo ya kupinga ukatili wa jinsia inaendelea kutoa hudumakwa wananchi wa Mkoa huo ambao wananchi wake wameipokea vyema kampeni ya Mama Samia Legai Eid.

Amesema kuwa hadi kufikia jana tayari wapo ndani ya malengo ya kuwafikia wananchi zaidi ya 60,000 na kwamba hadi kufikia Agost 1 mwaka huu ambayo ni siku ya kilele ya kampeni hiyo mama samia legal eid watakuwa mavuka lengo .

Dkt. Ndumbaro amevitaka vyombo vinavyosimamia kutoa haki vione umuhimu wa kutoa haki kwa kuzingatia maadili ya kazi na kwamba watoa maamuzi wsanapotenda kazi zao za kila siku wanapaswa kuzingatia haki na sio kuonesha upendeleo kwenye maamuzi ili wananchi wasiwe na mashaka pale anapopata huduma kwenye vyombo vinavyosimamia haki.

‘Mara baada ya uzinduzi ule timu ya wataalamu ilisambaa mkoa mzima wa Ruvuma walikwenda kila kona wamewafikia wananchi wengi sana na wamefanikiwa kutatua migogoro mingi sana ,wananchi wengi wa mkoa wa Ruvuma wameipokea vizuri sana kampeni hii wameshukuru sana na wameishukuru serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwalete kampeni hiyo ambayo inatoa elimu ya kisheria na msada wa kisheria kwa wananchi.’’alisema waziri Dkt. Ndumbaro.

Aidha Waziri Dkt. Ndumbaro amewataka watoa maamuzi kutokalia mafaili na kuacha kutoa maamuzi kwa kuchelewesha bali watoe maamuzi kwa wakati na kuacha kutoa maamuzi yanayomkandamiza mwananchi ambaye ni mnyonge kwa sababu mbalimbali na mtoa maamuzi atakaye zingua serikali itamzingua na si vinginevyo.

Hata hivyo waziri wa sheria na Katina amevipongea vyombo vya habari kwa kazi nzuriya kuendelea kutoa hamasa tangu kampeni hiyoilipozinduliwa na makamu wa Raisi Dkt. Pholip Mpango Julai 21 mwaka huu na kwamba zoezi hilo la kampeni ya kutoa elimu wa ukatili wa kijinsia utakuwa endelevu.

Kwa upande wao wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameishukuru Serikali kwa kuwaletea kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama SAMIA 2023 HADI 2025 kwani wengi wao wameweza kutatuliwa migogoro mbalimbali ikiwemo ya Ardhi,Ndoa na Mirathi.

Kampeni ya kitaifa ya msada wa kisheria ya mama samia tayari imetekelezwa mikoa minne hadai sasa ikiwemo Dodoma, Manyara,shinyanga na sasa Ruvuma .

Please follow and like us:
Pin Share