Za8di ya silaha za kijadi aina ya gobore 150 zinazomilikiwa kinyume na sheria zimekamatwa katika ijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga .
Hayo yamesemwa na MKuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya kijiji cha Msomera mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba.
Amesema kuwa ukamati huo unatokana na oparesheni wanayoendelea kuifanya ya kuhakikisha eneo hilo linaendelea kuwa katika hali ya usalama na amani .
“Ni desturi ya wananchi wa huku kwetu Handeni kupewa gobore kama zawadi wakati wa kuzalisha hivyo tumewaelimisha na Sasa tumeanza kuzichukuwa silaha hizo Ili kuimarisha usalama wa eneo hili”amesema DC Msando.