Vijana wametakiwa kuacha tabia ya kuuza viungo vyao vya mwili ikiwemo figo ili kuepukana na madhara ya kiafya.

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa wito huo akiwa ziarani mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua jengo la kutolea huduma ya usafishaji figo lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph–Peramiho.

Dk Mpango amesema utoaji wa figo unaweza kuhatarisha maisha hususani figo iliyobaki inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Aidha, amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kuepukana na hatari za maradhi mbalimbali na kufikia hatua mbaya zaidi.

Dk Mpango ameshauri kuachana na ulaji usiofaa, unywaji wa pombe kupitiliza pamoja na kuhimiza kufanya mazoezi kuepukana na hali hiyo.

Please follow and like us:
Pin Share