Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba wamefika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya zao na kufanya vipimo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya ya mashindano ya ligi 2023/2024.
Daktari wa Timu ya Simba Dkt. Edwin Kagabo amesema kuwa lengo la kuja kufanya uchunguzi Muhimbili Mloganzila ni kujua hali ya wachezaji wao kiafya kabla hawajaanza kupatiwa mazoezi ya msimu mpya.
“Kwetu sisi kama idara ya tiba na afya msimu wetu ndio umeanza, tumekuja katika hospitali hii kufanya uchunguzi wa afya ambapo tutafanya vipimo mbalimbali na tutajikita zaidi katika kuangalia mafuta mwilini pamoja na uzito kwasababu hivi vyote kwa namna moja au nyingine vinaweza kuathiri performance ya wachezaji wetu hivyo ni muhimu tujiridhishe kabla ya kuanza msimu huo” Amesema Dkt.Kagabo
Vipimo vilivyofanyanyika ni X-Ray ya kifua uchunguzi wa damu, utendaji kazi wa moyo kwa kufanya kipimo cha ECG, ECO pamoja na kipimo cha Ultrasound.