Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM )ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichotanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM leo, Julai 09,2023 katika Ukumbi Wa (White House) Jijini Dodoma .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 9,2023 Jijini hapa Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama hícho Sophia Mjema amesema pamoja na mambo mengine halmashauri Kuu ya CCM(NEC) imepokea na kujadili Kwa kina taarifa ya makubaliano ya Uwekezaji na uendeshaji wa bandari .

Aidha kamati hiyo imeazimia Uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni Kwa manufaa ya uchumi wa nchi na kwamba ni utekelezaji wa vitendo wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 Hadi 2025 ibara ya 59 ukurasa 92.

Ameyataja makubaliano mengine kuwa Serikali kutakuwa kuongeza Kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliopo kwenye makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari.