Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA), mkoani Mtwara aliyetambulika kwa jina moja la Regan amekufa baada ya kujinyonga kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na ugomvi wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuahidi kutoa taarifa kwa kina mara baada ya uchunguzi wa madaktari kukamilikwa.
Kamanda Katembo amesema kuwa mwili wa marehemu ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa wa chuo cha TIA na mkazi wa Mtaa wa Chikongola, Manispaa ya Mtwara- Mikindani mwili wake ulikutwa ndani ya chumba chake.
Amesema maiti imehifadhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Ligula kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujimu wa mashuhuda wamedai kuwa taarifa za kifo chake zilianza kusambaa jana Julai 4,2023 majira ya saa 6,mchana kwani siku moja kabla ya kifo chake alikua amegombana na mpenzi wake waliyekuwa wakiishi pamoja.
Kabla ya kifo chake marehemu Reagan aliweka picha yake ya utoto kwenye WhatsApp Status yake na kuandika maneno yafuatayo ——> “🙏🏾 kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa, maana WEWE NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI”