Na Andrew Chale, JamburiMedia, Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi wa Makamu wa pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika usiku wa tuzo za Tamasha la Filamu la Kimataifa la Nchi za Jahazi [ZIFF] kwa mwaka 2023.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Tamasha hilo la ZIFF, Profesa. Martini Mhando amesema wanatarajia kuwa na Hamza ambaye atatoa neno pamoja na ukabidhi wa tuzo kwa washindi.
‘’Hadi kufikia jana Julai 1, 2023 tumeweza kuonesha filamu 90, katika maeneo mbalimbali ikiwemo Unguja na Pemba.
Watu mbalimbali wameweza kuzipokea filamu hizi ambazo zinaburudisha na kuelimisha pia.
Hivyo basi jioni ya leo Julai 2, utakuwa ni usiku maalum wa tuzo za ZIFF, ambapo filamu zilizofanya vizuri zitatunukiwa.” amesema Prof. Mhando.
Aidha, amezitaja baadhi ya tuzo zinazotarajiwa kutolewa jioni ya leo kuwa ni za vipengele vya:
Filamu ya mwigizaji bora wa kiume, Mwigizaji bora wa kike, Best Feature Film, Lifetime Achievement Award, Tuzo za Ziff, Filamu bora fupi ya Ziff, Best Documentary – silver Dhow, filamu bora Tuzo ya dhahabu, tuzo ya Wakf ya Emerson na zingine.