Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma..
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi,ameagiza waajiri wote wanawasilisha taarifa za kustaafu kwa mtumishi wake Katika kipindi cha miezi sita kabla ya kustaafu ili kuwapunguzia mateso ya ufuatiliaji mafao.
Katambi, amesema hayo leo Juni 20,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto wanazokutana nazo baadhi ya wanachma na wastaafu wanapofuatailia mafao kwenye mifuko ya pesheni.
Ili kuondokana na kero hiyo ameelekeza kila mfuko uhakikishe mwanachama analipwa ndani ya siku 60 za kisheria kwa wanachama wote ambao nyaraka zao zimewasilishwa kwenye mfuko kwa ukamilifu.
“Kutokuwasailisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ni kosa kisheria, michango iwasailishwe kwenye mifuko bila shuruti, waajiri wasiotoa mikataba kwa wafanyakazi wao ni kinyume na sheria ya ajira na mahusianao kazini Na. 6 ya mwaka 2004”amesema
Aidha ameagiza wakurugenzi wakuu wa mifuko ya pensheni ya PSSSF na NSSF kuhakikisha waajiri wote wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wastaafu nchini.
Katambi amesema anafahamu changamoto iliyopo kwa baadhi ya waajiri kutowasilisha michango au kuwasilisha michango pungufu ya watumishi wao pamoja na kuvunja sheria kutowasilisha michango na kupelekea usumbufu kwa wastaafu.
“Nawaagiza waajiri wote wanalipa na kuwasailisha madeni ya michanago ya watumishi wao kila mwezi, kila meneja wa mkoa awasilishe majina ya waajiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo”amesema Katambi