Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Shirika la Akili Platform Tanzania linalojiusisha na afua ya Afya ya Akili, mazingira na haki za binadamu Tanzania leo Juni 5 , 2023 Siku ya Mazingira Duniani wameshiriki kwa vitendo katika kutunza mazingira kwa kufanya usafi na kufundisha vijana na wenye ulemavu wa pamoja na wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa akili wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Lengo kuu ni kuinua uchumi wa vijana na watu wengine wenye ulemavu Tanzania kupitia kazi za mikono.

Mkurugenzi wa Shirika la Akili Platform Tanzania Roghat Robert ametoa elimu juu ya afya ya akili kwa watu wenye ulemavu na wanandoa kwa ujumla kwa kuusisha na suala la mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathari binadamu.

Mkurugenzi huyo ameomba Watanzania kuendelea kuungana katika kuwezesha shirika hilo katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa mazingira nchini.

Pia ameishauri jamii kujikita katika kilimo miviringo (mbegu za karoti, Beetroots, papai, pilipili, na mazao mengine) ili kuchangia kusaidia wenye ulemavu wa akili kupitia kilimo hicho.

Mkurugenzi wa Shirika la Akili Platform Tanzania Roghat Robert

Amesema kuwa shirika litaendelee kuwafikia VIJANA hasa wa vijijini kwani wengi hujikuta katika matatizo yanadhuru afya ya akili kama dawa za kulevya, sigara, pombe na kujiingiza katika makundi ysiyofaa.

Naye Katibu wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Akili Wilaya ya Nzega, Daud Yassin ameomba kuwepo kituo cha ushauri na unasihi mkoa wa Tabora Wilaya ya Nzega kwani huduma iyo haipo.

Naye John Poneka ambaye ni mwenyekiti wa CHAWATA Wilaya ya Nzega ameomba kuwepo kwa kituo cha mazoezi ya viungo na semina ya Aya ya Akili kwa watu wenye ulemavu itolewe zaidi maana wengi wanashida ya utegemezi kupitia walivyo.

Hata hivyo mkurugenzi Roghat F Robert WA APT amesema yuko tayari kuungana na nao katika hali zote kuhakikisha anaondoa umasikini wa fikra kwa watu wenye ulemavu na mitazamo hasi.

Pia suala la kituo cha ushauri na unasihi analifanyia kazi ili huduma itolewe kwa vitendo.

‘Tazama Tafakari Tenda kwa busara tunza afya ya akili na Mazingira ulipo ‘

Please follow and like us:
Pin Share