Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt.Angelina Mabula amegeuka mbogo na kuwashambulia watendaji wake akiagiza,hataki kuwaona ofisini wale wote waliolalamikiwa kuhusika na migogoro ya ardhi iliyokithiri mkoani Dodoma ambapo Wizara imebaini wananchi wengi, wabunge 20,mtumishi wa TAKUKURU na taasisi za dini na umma, wameporwa na kutapeliwa viwanja ilihali wamelipa mamilioni ya fedha.
Dkt.Mabula amesema hayo Aprili 25, 2023 akisikitishwa na watalaam wa sekta ya ardhi wanaotegemewa na Taifa wakisaidiwa na baadhi ya viongozi wenye mamlaka,kuhamisha makaburi na kupima viwanja.
Akizungumza katika kikao kazi na watalaam hao kilichohusisha,safu ya viongozi wa Jiji la Dodoma akiwemo Mkuu wa Mkoa, Rosemary Senyamule, Dkt. Mabula ametoa taarifa ya kamati iliyoundwa na Ofisi yake Septemba 2022 kusikiliza kero za migogoro ya wakazi hao na kubaini wananchi wengi wameporwa na kutapeliwa viwanja.
Aidha Waziri Mabula amekasirishwa kuona ramani za mipango miji zilizochorwa na ambazo utekelezaji wake bado haujanza kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, mapumziko na mito, zimebadilishwa na kupimwa viwanja vya maduka ya biashara, migahawa na Sheli, ambapo wakazi wa Dodoma wamempongeza na kudai wamesikia kufokafoka kwake ila kuwe na matendo siyo kiini macho cha kubebana.
Alisema kwa siku (8) Kamati ilipokea watu 2511 na malalamiko 815 ya mkoa na wilaya za Dodoma, chanzo kikiwa ni watendaji kukosa uadili, udanganyifu wa madalali na wafanyakazi wanaojitolea, na ilibainika badala ya watalaam kutatua migogoro wanaiongeza, kwa sababu ya udhaifu wa usimamizi wa sheria za ardhi, kukosekana kwa uadilifu na wafanyakazi wanaojitolea, kuwa ni taarifa itakayowasilishwa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa na wilaya.
Alita tamaa ya fedha kwa watendaji imesababisha kumegwa hata makaburi ya kilimo kwanza na kuonya ‘watafufuka kule chini’ halafu mtashangaa jambo kumshitusha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweli iwapo yanafanywa yanatendwa na watalaam, ambao hata Makazi ya viongozi wamepima mabaa, migahawa na maduka, wakati jiji linadaiwa na watu fidia bil. 3/- na kuagiza Mkurugenzi na timu yake watimize wajibu wao.
Mbali ya kumshukuru mpima ardhi wa mkoa wa kwa kukataa upimaji huo na kumpongeza mkuu wa wilaya hiyo ‘Shekimweri’ kwa kutoridhishwa na madudu ya watalaam hao Mbabula aling’aka, “Mimi kama Waziri mwenye dhamana sipo tayari kuona Dodoma inaharibika, na ndiyo maana nilitaka wakurugenzi wote wawepo ili wakachukue hatua”.amesema.
Hata hivyo aliinyoshea kidole ofisi ya RAS akidai haiwasimamii viongozi wake kwa sababu nia nzuria ya Rais Samia Suluhu ya urasimishaji wa ardhi haikuwa kudhulumumu ardhi za watu, kuchukua fedha zao, kuwafanya wananchi maskini au kuwaacha na kilio, hivyo ieleweke wasiowajibika wanamgombanisha Rais na Wananchi na wanaigombanisha Serikali na watu wake na kuifanya itukanwe kwa uzembe wa baadhi ya watalaam na wenye mamlaka.
“Wananchi wanalia Wakurugenzi na Madiwani mpo! Hamchukui hatua! Mnataka waziri ndiye aje kuvunja uasi na uovu mlioufanya? Mnataka niwe sehemu ya wale waliofanya uovu wa mambo hayo?
“Sitaki kuona uasi huo unafanyika kwenye uongozi wangu labda kwa mwingine atakayekuja lakini kuidhinisha viwanja vya 20/20, kubadilisha mipango ‘plan’, kuidhinisha viwanja vilivyopimwa kwenye makaburi sifanyi.
“Je aliyelala kule chini anafurahia? Mianya ya tamaa ya kumega makaburi ya kilimo kwanza, imewafikisha hapo! Watafufuka kule chini halafu mtashangaa! Na hii ndiyo maana Shekimweri alichukizwa maana yanayofanyika si ya watalaam ambao hata makazi ya viongozi wanapimwa mabaa, migahawa na maduka, “Mkurugenzi na timu yako timizeni wajibu wenu”.
Waziri alitaja mifano ya baadhi ya watu na taasisi zilizopowa na kutapeliwa viwanja na watendaji wa sekta ya ardhi ya Halmashauri ya Jiji kuwa ni pamoja na Kiwanja Na.60 Kitalu ‘S’ Iyumbu cha AICC waliolipa mil. 200/- lakini kiwanja hicho amepewa mtu binafsi.
Aidani Mjwausi aliyelipa fedha zote taslimu mil. 182/- kiwanja chake amepewa mtu mwingine ikidaiwa atapewa mbadala, huku mtumishi wa TAKUKURU ambaye waziri anamshangaa kwa nini hajawashughulikia, alilipa malipo yote lakini ametapeliwa kiwanja akiahidiwa kupewa mbadala, na waziri kushitushwa na wafanyakazi wanaojitolea kuwa na magari na majumba.
Katika toleo la Jumanne Machi 28 – Aprili 3-, 2023, JAMHURI lilimtahadharisha Waziri Dkt. Mabula asitegwe na watendaji wake waovu kurasimisha Uasi wa Sekta ya Ardhi wa Halmashauri ya Jiji hilo, unaofanywa makusudi na watendaji hao kupora na kupima viwanja vya wanyonge na kuwapa vigogo ambao hujenga usiku na mchana ili avirasimishe kwa maana ya walalahoi wasubiri kupewa viwanja mbadala ‘badala ya kuvunja’ wakibainika.